Vurugu kumpinga Rais Kabila DRC

Vurugu kumpinga Rais Kabila DRC

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,086
Reaction score
34,883
150106111702_joseph_kabila_drc_512x288__nocredit.jpg

Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001
Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.

Serikali inasema kuwa watu wanne walifariki katika vurugu za Jumatatu ingawa upinzani unasema idadi huo huenda ikwa kujuu kuliko iliyonakiliwa.

Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhjudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.

Wanatuhumu wanasia wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila ambaye muhulka wake wa pili unatarajiwa kumalizika mwaka ujao kwa kujaribu kujiongeza muda mamlakani kwa kuidhinisha mipango ya kufanyika sensa ambayo itachelewesha uchaguzi kwa miaka mingi.

Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.


150120114313_drc_moto_512x288_bbc_nocredit.jpg

Waandamanaji wanamtuhumu Rais kwa kufanya wanachokiita mapinduzi ya kikatiba

Vijana walioandamana kwa vurugugu, waliteketeza magurudumu ya magari, kupora maduka na kurusha mawe.

Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.
Walisema polisi walingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.

Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba.

Mswada huo unapendekeza kufanytika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.

Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba.


Chanzo:BBC
 
Hawa ndio Viongozi Wa nchi jiran DRCi!

Hata Burundi kwa Nkurunzinza ni fujo pia kwa sababu hizo hizo!

Sisi hapa Tz hatutaki tu wimbi la wakimbizi wengine tuna matatizo yetu kutosha!
 
Ndio wale wale, wanataka kutawala milele. Tanzania pia ndio wale wale tofauti Tanzania is de facto single party dictatorship.
 
dogo angeachia ngazi mapema akiendelea hivi ICC inamngoja.
 
huu ukanda lazima usafishwe na viongoz sampuli hii, kuna huyu jamaa kabila, kuna nkurunziza, kuna kagame na mwenazo museven sijui ndo wanaiga kutoka kwa museven!!!! they need to go no wonder dunian watu wa maeneo haya ndio maskini kabisa!!!
 
Back
Top Bottom