Hii nchi haina serikali? mbona watu wanajichukulia sheria mkononi siku hizi? ajali za barabarani ni kitu kinachoweza kutokea sasa inakuwaje watu wanaona kama kitu kisichoweza kutokea? Ninavyojua serikali ni chombo cha kuogopewa na kuheshimiwa, kazi yake kubwa ya ndani ni kusimamia sheria kwa kutumia vyombo vyake vya dola ikiwemo polisi na mahakama, sasa hawa raia wanaoamua kuziba barabara inakuwaje? kwani mahabusu zimejaa Tanzania?