Vunjo tumepata mbunge awamu hii

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Mimi ni mkazi wa jimbo la vunjo natoka kijiji cha lyasongoro kata ya marangu mashariki tarafa ya vunjo mashariki ambayo makao makuu yake yapo kata ya mamba kusini wilaya ya moshi, mkoa wa kilimanjaro.

Nimesoma shule ya msingi lyasongoro na sekondari kidato cha kwanza mpaka cha nne darajani sekondari maarufu kama shule ya mazoezi kwani wanafunzi wa chuo cha ualimu marangu ndipo wanapofanyia mafunzo ya vitendo. Kidato cha tano na sita nikasoma shule ya wavulana tabora na baadae nikajiunga chuo kikuu cha dar es salam shahada ya siasa na utawala niliyohitimu mwaka 2009.Hivyo Vunjo ninaifahamu vizuri.

Nimepiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 2000 nikamchagua meja mstaafu Jesse Jeremiah Makundi kutoka chama cha TLP bahati mbaya akatuangusha.

2005 tukamchagua Aloisi Kimaro wa CCM marehemu kwa sasa ambae alijitahidi kufanya kazi japo siasa za makundi ndani ya CCM zikamuangusha na kuiangusha CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hali ikaendelea kuwa mbaya kwani alichaguliwa Agustin Lyatonga Mrema lakini naye akachemsha vibaya.

2015 James Mbatia akashindia upepo wa ukawa ila akawa moja ya wabunge waliofanya vibaya kuliko wote kwenye historia ya jimbo hilo kwani kwenye uchaguzi wa 2020 alipata kura elfu 4 tu kati ya wapiga kura zaidi ya 50 elfu.

Tuache utani kwa sasa mwanga umeanza kuonekana vunjo huyu dr kimei ni matumaini mapya. Kwa mara ya kwanza mbunge anarudi kushukuru wananchi, anarudi kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni zaidi ameweka ofisi jimboni ambayo ameweka mtu muelewa anajua mambo mengi ndg msiga jamaa sio mwenyeji wa huku lakini ana utulivu sana kwenye kusikiliza watu.

Ndio maana nasema vunjo tumepata mbunge. akiendelea na kasi hii 2025 wananchi watamchukulia fomu. Kimei anaipenda sana vunjo yaani anaihudumia kama familia yake.

Hakika unaiga vyema nyayo za JPM kwenye kuwatumikia wananchi.
 
Atakuwa anatumia akiba yake ya CRDB (anarudisha kwa jamii) maana tunajua fedha ya maendeleo ya jimbo hazitoshi kuleta maendelea kwenye jimbo zima. Namtakia kila la heri.
 
Amekuahidia ngapi?? Mnapenda kweli kujaza sever. Hata mwezi bado tiyari ushaanzakampeni ya 2025!!!! Jamaniacheni ujingaaaa
 
Sawa msemaji wa huyo Dr. Kimei. Tumekusikia. Ila kwa mtazamo wa wengi, muda wa kampeni bado sana. Kwa sasa mshauri mbunge wako ajikite zaidi kwenye kutekeleza ahadi zake. Halafu hizi kampeni utazianza mwaka 2025!

Nb: Usirudie tena kuuongelea uchaguzi wa mwaka 2020! Unapata wapi ujasiri wa kuyaongelea yale maigizo hadharani?
 
Mimi ni mkazi wa jimbo la vunjo natoka kijiji cha lyasongoro kata ya marangu mashariki tarafa ya vunjo mashariki ambayo makao makuu yake yapo kata ya mamba kusini wilaya ya moshi, mkoa wa kilimanjaro.
Bila jina kamili na namba ya simu habari hii haitanoga
 
Mbunge ambaye sio Waziri, na hana wadhifa ktk chama, anatakiwa aishi pamoja na wananchi wake jimboni.
 
Back
Top Bottom