Vulnerability

Vulnerability

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,490
Reaction score
8,305
Mko salama watu wangu..
Naomba nijadili kwa ufupi tu hilo neno hapo juu. Nimegundua kuwa binadamu wengine ni vulnerable (rahisi kuumia) kuliko wengine. Kuumia huku ni kwa aina tofauti mfano kihisia,kisaikolojia,kifizikia ila yote no kuumia tu. Watu vulnerable wanatabia hizi hapa.
1:Wanatamani kutendewa na watu vizuri lakini hawamtendei mtu vizuri.
2;Wakifikwa na janga wanalalamika sana kama vile majanga hayatakiwi kuwapata.
3:Hutamani kuheshimiwa sana ila hawaheshimu wengine.
4:Wanaamini Mungu yuko karibu nao sana kuliko wengine.
5;Wanapenda kutambuliwa uwepo wao hata kama siyo muhimu.
6;Ni wepesi wakusahau maneno na matendo yao.
7;Wanaamini mawazo yao ni sahihi siku zote,Hawapendi kabisa kukosolewa.
8:Hupenda sana kusifiwa kwa gharama yoyote ile.Yaani ukifanya kitu kizuri wanakwambia hilo ni wazo langu nililitoa siku nyingi.Umeiba idea yangu.
9;Hawapongezi mtu ng'o..kwao kila kitu kina kasoro za kurekebisha.
10:Wakiamini jambo wameamini hata ungefanyaje,wakipenda wamependa,wakichukia wamechukia.Hawataki kabisa kuambiwa totauti.
Kama una tabia hizi kuanzia nne na kuendelea uko katika hatari ya kupata msongo (depression) au weweseko (delusion).


Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom