Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,608
- 93,382
ritz labda nikusahihishe, hilo jimbo la Ukonga linaongozwa na mbunge wa CCM Mwanamke mmoja anaitwa sijui Eugine Mwaiposa, pili hiyo kata kunakofanyika huo mkutano Diwani wake ni Jery Silaa na ambaye ndio meya wa Ilala, sasa nashukuru kwa kutupa taarifa kwamba kumbe kata anayoishi meya wetu hata barabara ni mgogoro, kwahiyo Mimi kama Matola mkazi wa jimbo la Segerea sitegemei maendeleo yoyote kutoka kwa viongozi hawa wa CCM.Nilikuwa nataka kuja kwenye huo mkutano nimeishia pale Moshi bar nimerudi barabara mbovu sana...jimbo la Matola
Mkuu usichanganye.Mkutano wa leo upo hapa Ukonga mazizini na mkutano wa Jumamosi ni wa kitaifa Jangwani.Nipo mkutanoni nitawapa updates kadiri inavyowezekana.
Suala la kutimuliwa shibuda haliko simpo kama wengi wanavyoweza kuamini. Tujifunze kutokana na yaliyojiri kwa akina Hamad Rashid na Kafulila.Wadau mniwie radhi kwa kutowapa updates, nilikuwa na majukumu ya kusimamie protocal ya mkutano.
UKONGA YATAKA SHIBUDA ATIMULIWE!
Katika hali ambayo haikutarajiwa viongozi pamoja na wanachama wote wa Chadema waliohudhuria mkutano wa leo wametoa msimamo wa kutaka John Shibuda atimuliwe ndani ya chama mara moja.
Wamemuomba Mh. Suzan Kiwanga afikishe salamu hizo kwa uongozi wa Taifa na hatua ichukuliwe bila kumuonea aibu.
Sorry, walipambana kivipi mkuu!Amepanda Henche,anamtambulisha kijana aliyepambana na Lusinde kule moro anaitwa Lamerk, na umeme umeleta tatizo kidogo
Kwa sababu huu mkutano unafanyika Dar natarajia updates ziendane na mafoto.Susan Kiwanga: serikali ya ccm kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi raisi ni mafisadi.
Kiwanga: kwa mujibu wa ripoti ya CAG raisi kikwete anavunja sheria na kukiuka kanuni za ajira kwa kuwateua wanajeshi kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, wanalipwa mishahara na malipo yote stahiki ya kisiasa lakini wakati huo huo wanalipwa stahiki zao katika ajira zao za kijeshi.
Huu mkutano ni muhimu sana kwa wakazi wa Dar na watanzania kwa ujumla.Mwita Waitara: Katiba mpya si agenda ya ccm kwahiyo wameiteka agenda ya Chadema na kutaka kuwalaghai na kuwazuia wananchi kujadili na kutoa maoni yao bila vikwazo. Wananchi wawe huru kujadili juu ya nchi yao bila masharti.
Jumamosi ijayo 26/05/2012 kutakuwa na mkutano mkubwa Jangwani na viongozi wa taifa watatoa tamko la muelekeo na msimamo wa chama katika katiba mpya.