Vodacom tz kwafukuta..

Ngoja na mimi nikopi format ya hii barua kuna wajinga flani wananisumbua hapa job
 
Deal na kutajirika haraka haraka...halafu wenye mali waliamua vingine tunawaona wanga. Kitu cha msingi ni kwa muajiri kufuata taratibu zote za kisheria...ila duka la mtu ni la kwake tu. Anaweza kuamua lolote analotaka.

Kama anauhuru huo mwambie mwenye duka achague nchi siyo Tanzania
 

Wafanyakazi wa voda kama ni wezi wapelekwe kwenye vyombo vya sheria na isiwe kigezo cha kuhalalisha kuajiri foreigners wengi hii haipo sehemu yoyote duniani.
 

chukua tano
 
Ndilo tatizo letu watanzania. Mali ya wizi tunaiita mafanikio!!! Nilikuwa na hamu ya kujadili lakini sijadili tena.

Ndugu, uitazama post ya MdogoWenu uatgundua kuwa wafanyakazi wa Vodacom anaowafahamu wamepata mafanikio ndani ya kipindi kifupi.Tazama post anayozungumzia kumpangisha mfanyakazi wa vodacom mwenye nyjmba tatu sasa.
Kwa mtazamo wangu si sahihi kumuit ahuyo kijana ni mwizi kama uthibitisho uliokuwepo ni wa kimazingira.Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kumfanya huyo kijana kuweza kujenga nyumba tatu ndani ya miaka 8,na zinaweza zisiwe na uhusiano na vodacom.sidhani kama wafanaykazi wa vodacom wote wameweza kujenga nyumba 3 katika kipindi cha miaka 8,kwani sasa wanahukumiwa kwa makosa waliyofanya wachache,kama kuna ubadhirifu washughulikiwe wabadhirifu,kama hao VODACOM/NSN ni wazembe kiasi cha kushindwa kuwafahamu wabadhirifu,basi wasiweke mzigo wa uzembe wao kwa kuwaajiri wageni kwa kuvunja sheria za nchi.LINAPOKUJA suala la uvunjifu wa sheria za nchi,hutakiwi kuweka visingizio vya fulani mwizi n.k.Taratibu za kuwashughulikia wafanyakazi wezi/wabadhirifu zinafahamika.huu ujumuishwaji wa kiholela.ili mradi watekeleze sheria za kikandamizaji si sahihi.
 

Wizi uliosemwa na huyu bwana MdogoWenu hauna proof,ingekuwa vizuri angewataja kwa majina,ikiwezekana akaandika na Barua kwa uongozi wa juu wa NSN an VODACOM,akiambatanisha kwa wakuu wa usalama wa nchi hii,kama kweli ana ushahidi wa kutosha wa wizi huo.mbali na hapo si busara kuwaita wafanayakazi wote wa vodacom/NSN wezi kwa kusikiliza kauli tupu ya mheshimiwa aliyeandika kwenye jamiiforum.

kwa upande mwengine, malalamiko ya hao wafanyakazi ni jambo la ukweli na lililothibitishwa kwa barua waliyoiandika na majina ya hao wahusika.sio tatizo la kufikirika au la kudhanika.
Hili ndio tatizo la kujadili kwenye mada,kwani liko wazi na viambatanisho vimewekwa.

Mdogowenu kama kweli ana uchungu na wizi unaofanyika na hawa wafanyakazi wa VODACOM/NSN si vibaya akafungua mada ili tuchangie kwa kufuatisha vielelezo vitakavyowekwa
 

kwa kampuni kama NSN kitengo kimoja kuwa na wafanyakazi 15 wa kigeni sio jambo zuri.kazi wanazofanya Tanzania sio kazi zinazohitaji uwe umetokea ufini yalipo makao makuu ya NSN.na kwa kutazama asili ya majina yale wafanyakazi 9 wana asili ya india/pakistani waliobaki ni waafrika ya kusini na wazungu,hakuna jina lenye asili ya ufini.

ukija upande wa kiufundi,tecknolojia haiko hivyo,kufanhamu ujuzi wa "switching" n.k si lazima utokee ilipotokea mitambo,ndio maana watu wanakwenda chuo kikuu kujifunza,kwa maana ya kuwa mitambo yote inatengenezwa kwa kufuata viwango vilivyo sawa dunia nzima.mhandisi mjuzi anahitaji mafunzo ya muda mfupi tu kuelewa vitu vichache vilivyo tofauti na viwango vinavyofuatwa dunia nzima.
 
Wewe haya madai yako yana proof gani. Barua yenyewe kwanza haina proof na hata haijulikani imeandikwa na nani!!

nadhani wafanyakazi wa NSN ni uthibitisho tosha imeandikwa na nani.uthibitisho mwengine ni majina ya hao wafanyakazi wasio watanzania huko NSN
 

hawa wafanyakazi wa NSN wameleta malalamiko yao kuhusu upindifu wa sheria kwenye ajira za wageni.wewe unaongelea biashara za viwanja,huoni kuwa wewe ndio unapotezea mada yao?

mtu akileta mada kuwa wafanyakazi wa ardhi wanaonewa a,b,c watu tukianza kuelezea kuhusu rushwa iliyokuwepo wizara ya ardhi tutakuwa sahihi?je kila mfanaykazi wa ardhi ni mla rushwa?je wewe ni mla rushwa?

kama majibu ya maswali hayo ndio,je hustahili kulalamika pale unapoonewa?
 
Nimeuliza na hutaki kujibu. Unazungumzia kutaja mambo ya kiufundi wakati barua imetaja hadi menejiment na administrative posts. Taja watanzania mle Vodacom au NSN ni wangapi ili tujue, maana barua haitaji.

sifanyi kazi NSN wala VODACOM, sifahamu,naongelea mambo yaliyowekwa wazi,na sio yasiyokuwepo.au nisiyoyafahamu.
Tatizo hasa liko hapo kwenye hizo nafasi za uongozi wa kati,kwani ndio zinawaandaa wazawa kunyonya ufundi na weledi wa kuongoza mashirika ya kiufundi.wakitoka wakienda mashirika ya umma,hawataweza kuchukua ujuzi wowote wa uongozi,kama huko walikotoka hawakupewa nafasi.
 

Tanzania Hatuna Taratibu za kufuatilia uhalali wa vipato vya watu,mamlaka yetu ya Mapato haina weledi na uwezo kama wa IRS ya marekani,hivyo ni vigumu sana kuweza kuthibitisha mali za wahusika.
Tumeanza kuchukua hatua kurekebisha mfumo ili kuweza kufikia sehemu ambayo mali za mtu zinaweza kufahamika kirahisi,Mfumo bora wa Kodi,Urajisi wa ardhi,urajisi wa ukazi,urajisi wa mapato ya watu n.kmifuko ikikaa vizuri tutaweza kupambana na mafisadi pamoja na wezi wanaohujumu sehemu zao za kazi n.k

sijakataa kuna wizi kwenye makampuni,upo,ingawa mimi simfahamu mtu anayefanya kazi VODACOM na NSN,lakini ninachofahamu ni kuwa vyombo vyetu vya dola havina uwezo wa kupambana na wizi wa kimfumo bado.

binafsi msimamo wangu ni kuwa,kama kuna wafanyakazi wezi,washtakiwe,kama wewe una taarifa hizo zifikishe kwa viongozi wao huko VODACOM/NSN hapo utakuwa umesaidia kuondoa tatizo.

lakini kwenye hili suala la hawa jamaa wa NSN kuziba ajira za ndani kwa sababu ya wafanayakazi wezi ni kosa na wanapaswa walirekebishe
 

Vodacom imeingia hapa nchini lini. Nadhani ni mwaka 2002. NSN imeingia hapa nchini lini? SIna hakika lakini nadhani ni kabla ya 2005. Kwa nini madai haya hawa wazawa wa Vodacom na NSN wamekaa nayo miaka yote na sasa wanayaleta leo yaani 2012?

Ni wazi kabisa kuna jambo limetokea na hivyo wanakuja mitandaoni kupata moral support na kwa sababu hatujui kilicho nyuma wanajua watatuokota watanzania wengi tukurupuke kuwatetea kwamba wanatetea ajira zao.

Kama ni wingi wa experts basi wingi huo ulikuwa mwingi wakati Vodacom inaingia kuliko wakati wowote. Kitengo cha ufundi kilikuwa kinaendeshwa na SIEMENS na hakukuwa na mzawa hata mmoja.

Sijui kilitokea nini humo ndani ya kampuni hawa SIEMENS wakaondoa na wazawa wakawa wengi wakaajiriwa humo VODACOM na baadaye wakachukuliwa NSN.

Hivyo, kumbe hali ya wazawa kupewa nafasi ni kwamba walipewa SIEMENS walipoondoka. Leo hawa jamaa wa NSN wanakuja na madai haya ambayo huko nyuma waliweza kuyashughulikia humohumo ndani na wakafaulu iweje leo wasifaulu. Je, wamedhulumiana ufisadi sasa kila mtu anataka popular support humu mitandaoni?

Hivyo, tunatakiwa tutafiti hasa kilicho nyuma ya hili kuliko kukimbilia ushabiki ambapo tutajikuta tunatetea mtu na ajenda yake kama jinsi mle bungeni watu walikimbilia kutetea TANESCO kumbe kuna wabunge walikuwa wanafaidika na utetezi ule.

Akili kichwani!!
 
Haya sasa ndo majungu yaliyoenda shule. Cha msingi tupunguze uvivu na starehe halafu majungu haya tuyapanue mpaka kwa wale wazawa wanaotoa ajira kwa ukabila kama ITV..!
 
Kama anauhuru huo mwambie mwenye duka achague nchi siyo Tanzania

teh teh teh....hata wewe na mimi tukisema no, haina maana wataondolewa Tanzania. By the way, hilo ni duka lake kweli. Ana hiari ya kufanya anachotaka. Namna pekee ya kumbana ni kuwa na sheria zinazofuatiliwa na zinapewa meno ya kufanya kazi.
 

Unachosema kina ukweli kwa asilimia kubwa sana...ngoja tuone mambo yanavyokwenda.
 

Masikini watanzania. Poleni sana wafanyakazi kwa hayo yaliyowakuta kwa sababu hapo ndiyo mwisho wa ajira zenu. Malalamiko yenu yote ni sawa kumpigia mbuzi gitaa acheze kwa vile nchi hii ni sawa haina mwenyewe na ndiyo maana wageni kama hao wanafanya watakavyo kwa sababu na wao wanajua hakuna atakayewafanya kitu. Nchi kwa kukosa uongozi imara imekuwa kama jamvi la wageni. Unaweza kushuhudia wageni wanavyoingia na kuchukua wanachotaka na kutoka bila bughudha. Subirini bado kiama kinakuja siku si nyingi pale wakazi wote wa Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na kwingineko watakapoingia na kuchukua kuanzia ajira, ardhi, rasilimali zote kwa sababu milango imeshafunguliwa na viongozi wetu mazezeta. Ee Mungu tunusuru na janga hili.... Amen
 
Hapo penye bld inabidi waTZ tubadilike kwani inatujengea sifa mbaya ya WIZI.
 
Hii ishu ni very sensitive, lakini kwa serikali yetu hii legelege inayoongozwa na handsome dhaifu, tuesabu maumivu tu... Nchi imeshakosa muelekeo, tukiipindua hii serikali tunaweza kupata ufumbuzi....
 
yalikuwepo mengi tu mbona

1.Afrikings now brand fusion hawa nao walikuwa na mkataba na vodacom wa kusimamia sales nchi nzima ma walikuwa na staff zaidi ya mia lakini mkataba wao umekatishwa ghafla mapema mwaka huu na kundi kubwa la hao staff kukosa ajira!!!!


dada aliyeshindwa majungu ndani ya vodacom na kukimbilia UN

[h=1]Stella Kiwango[/h]


[TD="width: 134"] [/TD]
[TD="width: 538"] Stella Yinza Kiwango recently joined the World Agroforestry Centre in February 2012 as Director of Administration responsible for overseeing the administrative operations of the Centre as well as Human Resources.
With over twenty years of experience in similar capacities in both the public and private sectors, Stella joins the Centre from Vodacom Tanzania, where her major contribution was in the area of Human Resources and organizational capacity building. Prior to that, she worked with BP Tanzania, leading the Human Resources function in Tanzania and also part of a diverse global and regional team engaged in the harmonization of global HR policies and procedures across the company.
Before that, Stella started her career with the National Board of Accountants and Auditors where, as Administrative and Personnel Manager, she was instrumental to the institution's development and was a forerunner in enabling the organization to solicit and implement donor funded technical assistance projects related, among other areas, to administrative and human capital capacity building.
Stella holds a Master's and Postgraduate qualification in Economics and Social Studies from the University of Manchester, United Kingdom, where she majored in Development Administration.
[/TD]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…