Vodacom tz kwafukuta..

Serikali yenyewe hipi haswa ya kuwatetea na kulinda ajira ya waTanzania? Serikali hii ya rais kuongwa vipande vya suti!!!!.waongwa

Mkuu naamini wabongo wakisimama kidete na kila kampuni kupaza sauti about huu muongezeko wa wageni non-professional lazima itachuka hatua, tatizo hao wafabyakazi wenyewe wauza sura tu kazi kulalamika tuu basi. Huu Ujinga hata Kenya hawawezi kukubali, only kwa waajiriwa wa Tanzania(waoga sana). Heri ya sisi tuliojiajiri kwa kilimo kuliko manyanyaso ya wahindi njaa wa bongo
 
NSN mbona sio Vodacom? Hii ni separate company

Ishu ipo hivi...
makampuni mengi ya simu yameoutsource dept zao za technical(maintanance na operation), si Tanzania tu bali hata sehemu nyingine duniani..Vodacom Tanzania ni mfano mmoja wapo na wana mkataba na NokiaSiemens.
Hivyo mwenye jukumu la kuajiri wafanyakazi wa Technical mostly ni upande unaohusu telecom network ni NSN...using that advantage ndio huwa wanalundika wataalam wengi kutoka nje.
 
Yasemekana hali si shwari ndani ya Vodacom Tz hususan baada ya mkataba kati yake na Nokia Siemens Networks (NSN) kitengo cha Operations.

Labda Dr. Slaa akiwa rais...lakini nikiangalia waliokopiwa kwenye hiyo barua wote ni wale waleee!!..hosea, manumba,..tumeshawazoea..hakuna kitakachofanyika
 
Vodacom wamekuwepo Tanzania kwa zaidi ya miaka 10 sasa, ina maana muda wote huo hawaja-train watanzania kushika hizo nafasi? Hivi kweli inaingia akili hata 'Human resource manager anatoka nje ya nchi? Hakuna mtanzania anaweza kufanya hiyo kazi?

Pia bado sijaelewa ni kwanini hadi leo hii Vodacom hawana jengo lao wenyewe, bado wanakodisha! Are they planning to leave the country? Commitment yao Tanzania iko wapi? Wana wateja zaidi ya 10 million (simu) na hatujagusa M-pesa. Lakini bado wanapanga office!
 
Ukweli ni kuwa wabongo tunajua kazi ila ni wavivu na wezi kupindukia ndicho kinachowasukuma kutumia gharama kubwa kuleta expatriates toka nje ya nchi
 
Wazawa waliopo NSN au Vodacom watujuze basi tuelewe wanalilia nini???
 
Ukweli ni kuwa wabongo tunajua kazi ila ni wavivu na wezi kupindukia ndicho kinachowasukuma kutumia gharama kubwa kuleta expatriates toka nje ya nchi

Deal na kutajirika haraka haraka...halafu wenye mali waliamua vingine tunawaona wanga. Kitu cha msingi ni kwa muajiri kufuata taratibu zote za kisheria...ila duka la mtu ni la kwake tu. Anaweza kuamua lolote analotaka.
 

umetoa jibu la kueleweka. nyongeza,hatuna budi tukiri na tuone kama janga la taifa vijana wetu wengi kukosa uaminifu makazini na ni wavivu,na baadhi ni mabingwa wa vyeti vya kughushi.
 
Jamani hata Human Resource Manager hatuwezi??? this is too much!!
 
Tatizo la kuzoea mfumo wa sisi wote ni sawa na Afrika ni moja ndio inakotupeleka huku. Matokeo yake ni kulalama mwanzo mwisho. Inawezekana ni bado hatujaweza kukabiliana na mfumo wa ushindani. Tena mmesahau sio wahindi tu, kuna wakenya, Wa-Nigeria, Wa ghana, Wa Afrika- Kusini, Wa-Senegali, Wanyarwanda, Wa Congo n.k Suala ni sifa na uwezo wa kukabiliana na ushiindani. Kamwe usitarajie kwamba utapata favor kutoka kwa mtu katika hili kama hujitumi.Matokeo ya kupendeleana na ushikaji ndio yanayotucost mpaka kesho. Bora hata ya wageni ambao wanapiga kazi wakijua siku yoyote wakiambiwa wasepe wanasepa kwingine na siri kwao ni kujituma na sio ubabaishaji wa kijinga wa kujiamini kwamba nikiharibu fulani yupo wa kunilinda. HABARI NDIO HIYO
 
Hili suala si la Vodacom tu. Ni nchi yote imeoza. Serikali haifanyi kiti chochote cha maana katika hili. Tulishakosa imani na serikali yetu. Watu mtalizungumzia lakini hakuna mabadiliko yoyote. Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Kazi sioni wanachokifanya katika hili. Wenzetu wageni hawana nafasi hata kidogo. Wengine hata sifa hawana.

Hapa bila miujiza ya MUNGU hakuna kitakachoendelea.:eek2:
 

Jamani serikali iwasaidie hata kwa hili? Naona mkuu umeyamaliza. Hawa ndiyo wanaopiga kelele. kama kuna mtu anayefikiria kuwa alichokisema MdogoWenu ni uongo tafuta watu aliyo wataja waulizeni.

Hata Vodacom wenyewe wanayajua haya fika kabisa.

Nafikiri hao walio andikiwa barua wafanye utafiti wa kina, siyo tu kwamba ni Voda wanashida makampuni mengi yanajikuta yanatamani kuwafukuza watanzania kwa sababu za udokozi kama huu.

Jamani tutafanya wadogo zetu wakose kazi kula kidogo.
 

Kuwepo kwa ukweli katika haya uliyoandika, hakuondoi uhalali wa madai ya hawa wafanyakazi wa NSN.Serikali itumie Busara katika kutunza soko la AJIRA nchini,kwani kama mfumo unaotumia na NSN ukifanikiwa,wawekezaji wote watautumia,na muda si mrefu utaambiwa na wataalam wa ARDHI hapo WIZARANI hawahitajiki kwani muwekezaji ameleta WATAALAM wake wanaoweza kufanya kazi bila kuiba.

Kuiba ni tatizo linalotakiwa kutatuliwa kwa njia tofauti,sio ya kuwanyima wafanyakazi waliokuwepo haki zao za msingi,na kudumaza soko la ajira nchini
 

Mheshimiwa sifanyi kazi NSN wala VODACOM,sijawahi kufanya kazi kwenye makampuni hayo mawili,nimeandika kwa kutazama uhalisia wa tatizo na sio kwa kuegemea upande wowote.
Umeandika kama mtu mwenye hasira kali na wafanyakazi wa vodacom,kutokana na mafanikio ya muda mfupi waliyoyapata,kutokana na hilo itakuwa ngumu kuijadili mada hii kwa mtazamo huru.
Sijaandika matukio ya wizi yasifanyiwe kazi,nimeandika kuwa kama NSN wanavunja sheria za nchi suala hilo lishughuikiwe mara moja,kwani baada ya muda waajiri wa kigeni watajifunza kutokana na yanayotokea NSN na kuendelea kuwakandamiza waajiriwa watanzania.
 
majungu haya...kma haina signature za wahusika waliondika then ni majungu...kwanza kuna foreign expatriates??? sijaelewa au kuna local expatriates pia...hahaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…