Vodacom Tanzania ni wezi

Vodacom Tanzania ni wezi

Mndwyika.wetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
652
Reaction score
829
Nimenunua kifurushi cha mwezi mzima kuanzi tarehe 14 February, nilipata GB kama sijakosea 19GB, mpaka tarahe 29 asubuhi bado nilikuwa na salio la GB 16.3.

Kifurushi changu kinaishia tarehe 15 March.
Jana saa kumi na mbili jioni napata sms hii kutoka VODA “Your TSH35000 bundle balance has finished. Enjoy freedom to call or browse in a bundle. Dial *149*01#>Pinduapindua”

Nimewapigia voda mara tatu sasa wananiambia tatizo lako linashughulikiwa tutakujibu baada ya masaa 24.

Hivi VODA Tanzania wanatupa hizi huduma kwa hisani au sisi wateja tunazilipia na ni lazima tupate huduma tuliyolipia kwa wakati?

Nilinunua kifurushi number 4

IMG_3436.JPG

Salio kama linavyoonekana kwenye app yao wenyewe lakini wamenikatia internet. Kuna hatua yoyote ya kesheria naweza kuchukua? TCRA wanaweza kusaidia chochote hapa?

IMG_3437.JPG
 
Nimekua mteja wao kwa zaidi ya miaka 17, nafikiri mda umefika saaa kuhama. Tatizo ni kwamba number yangu inatumika kwa mambo mengi sana ndani na nje ya nchi, naomba ushauri
 
Nimekua mteja wao kwa zaidi ya miaka 17, nafikiri mda umefika saaa kuhama. Tatizo ni kwamba number yangu inatumika kwa mambo mengi sana ndani na nje ya nchi, naomba ushauri
Unaweza kuwasiliana na jamaa zako wa ndani na nje ,pia huduma zingine mfano Benk,Bima,majengo Tanesco n.k,unaweza kuwaambia kuwa umebadilisha namba,usichelewe mpaka jioni uwe umeshawahama hao Vodafisi,
 
Voda ni wezi... Mtu una weka salio la 2500 ujiunge kifurushi wanakuambia salio lako halitoshi, mpk uongeze 500 ndy inakubali
Huu ni uwizi mkubwa wanaoufanya hawa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe umeona kwenye bando tu, kwenye miamala ndo usiseme laki mbili unakatwa 5,300 yaani M-Pesa ni tatizo wameongeza sana, mamlaka zifatilie hili jambo wanaumiza wnanchi na makato.
 
Nimekua mteja wao kwa zaidi ya miaka 17, nafikiri mda umefika saaa kuhama. Tatizo ni kwamba number yangu inatumika kwa mambo mengi sana ndani na nje ya nchi, naomba ushauri
Mkuu badilisha hiyo namba iwe ya mtandao mwingine... Yana namba zako hizo hizo lakini zinakuwa za Tigo..
Wapigie wakupe maelekezo
 
HAPA TATIZO SIYO VODA MKUU.

Tatizo ni TCRA nchi hii nihatari kukaa bila kuwa na kaofisi na wewe ka kupigia! Kila sehem mlaji wa mwisho niwizi mtupu! Watu ambao wamepewa dhamana ya kusimamia wananchi wamegeuka kuwa wapigaji kwa kuzitumia taasisi, makampui, wadau walio chini yao! Nenda kwenye mabucha! Kilo ya nyama nikama Robo kilo.

Nenda kwenye vyakula vyote vya nafaka iwe 100kg au 2kg lazima upigwe!

Kuhusu Bando za makampuni yte ya sim , cyo voda pekee yao! Sasa hivi makampuni ya simu yanashindana mbinu za kuibia wateja nasiyo kutoa huduma bora kwa wateja. Ndio maana mi sishobokei promo yyte ya makampuni ya sim, maana unaletewa promo lkn mwisho wake nikupigwa!

Mi nadhani NDG KILABA mkurugenzi wa tcra cjui bado yupo pale ajitafakari maana hilo nitatizo sugu!

Sehem nyingine ni gharama za kutoa pesa! Zimepandishwa mara dufu! Kutoka 200 nakuongezwa karibu600 kwenye kutoa elfu kumi .

Sehem nyingine ni kupangiwa matumizi ya kifurushi chako! Hii nayo cjaona haki! Kwanini isingekuwa kama umeme? Mtu unanunua unity zako utajua namna ya kujihudumia.

Hapa tatizo ni TCRA wanashirikiana na makampuni kutafuta GAWIO.
 
Duh Nilidhani nimepigwa peke yangu kumbe tupo wengi. Nadhani upande wa Internet Kuna shida
 
Voda mpenzi wangu badilika acha tabia ya kuwaibia wateja,huoni aibu unazomewa kila kona mwizi mkubwa wewe badilika na ukiri hadharani ulinde heshima yako ya kuwa mtandao bora.
 
Back
Top Bottom