Vodacom Premier League (VPL) Simba SC vs KMC FC, burudani ya uhakika Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Naaaaaaam,

Karibuni tena kwenye patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), ambapo leo March 1, 2020, mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama, wanawakaribisha KMC FC kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na wa kusisimua kwa pande zote huku Simba akisaka alama tatu muhimu ili kuweza kujihakikishia ubingwa kwa asilimia 100% na KMC FC wao wakitafuta alama tatu muhimu kuona kama watasalimika na hatari ya kushuka daraja.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amekiandaa vya kutosha kikosi chake huku akijiwekea malengo ya kushinda michezo minne iliyo mbele yake kabla ya ligi kusimama kupisha michuano ya CHAN, pia akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya uhakika kutoka kwa Simba SC.

Naye Kocha wa KMC FC, Hererimana amesema amechukua majukumu ya timu ikiwa katika nafasi ya hatari, na moja ya malengo yake ni kuhakikisha anaibakisha timu kwenye ligi hivyo basi, wanapambana kupata ushindi ikiwemo mechi dhidi ya Simba ili kuepuka kushuka daraja.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, Je leo mambo yatakuwaje? Tusubiri safari ya dakika 90 kuamua.

Kumbuka mchezo huu wa VPL utapigwa kuanzia saa 2:00 usiku, Usikose Ukaambiwa.

GHAZWAT

Kulitaka mwana, kulipewa mwana


==================
Update;

Klabu ya Simba imeweza kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania

Hadi kufikia mapumziko timu zote zilitoka uwanjani bila kufungana, kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake ambapo mpaka kufikia dakika ya 70 Simba walianza kuhesabu bao la kwanza kupitia kwa Luis Miquissone

Dakika mbili baadaye Luis Miquissone aliweza kutikisa tena nyavu za KMC baada ya kumalizia krosi nzuri ya Kada, kwa matokeo haya Simba ameendelea kujikita kileleni kwa alama 65 huku ikiwa imecheza michezo 25.

VPL, FT: Simba SC 2-0 KMC FC


IMG_20200301_105804_856.jpeg
IMG_20200301_112433_359.jpeg
67745844_452540995332307_221281863375347715_n.jpeg
 
Back
Top Bottom