Vodacom Premier League VPL | FT, VPL; Azam FC 1-1 Simba SC.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo kwa Viwanja tofauti, huku gumzo likiwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex ambapo Azam FC wanawakabili Simba SC.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati ameanza kwa kuwapongeza Simba SC kwa kuutwaa Ubingwa wa VPL huku akiongeza kwa kusema kuwa, mchezo wa leo utakuwa mgumu na licha ya ugumu lakini utakuwa nzuri.

"Mchezo ni mgumu lakini pamoja na ugumu wake utakuwa nzuri, na tumejiandaa kufanya vizuri ili kujiweka sehemu nzuri". Amesema Bahati.

Naye Kocha Msaidizi wa Simba SC Suleiman Matola amesema kuwa, timu itaingia uwanjani kwa kusaka ushindi pamoja na kuwa tumetangazwa Mabingwa wa VPL.

"Ni kweli tumeshinda ubingwa wa VPL, lakini haimaanishi kwamba tunazichukulia kawaida mechi zilizobaki, mechi dhidi ya Azam FC itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana ili kupata ushindi". Amesema Matola

Ni nani kuibuka kidedea? Usikose Ukasimuliwa kuanzia saa 1: 00 Usiku

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

..... Ghazwat...


==========

Naaaam wakati wowote mpira Utaanza Uwanja wa Chamazi Complex

Azam wapo uwanjani wakiwa wamejipanga mistari miwili na Simba kupita katikati ili kuwapa (guard of honour) gwaride la heshima kama Mabingwa wa VPL.

00' Naaaam mpira umeanza Uwanja wa Chamazi Complex | Azam FC 0-0 Simba SC.

05' mchezo umeanza kwa Kasi huku kila timu ikisaka ushindi mapema tu, mashambulizi yanaendelea.

10' Hakuna timu imeona lango la mwenzake, mpambano ni mkali Wanaume hawa wanapambana licha baadhi ya nyota kukosekana kwenye mchezo huu wa leo.

16' Free Kick kuelekea Simba..Azam wanapigaa lakini golikipa Kakolanya anacheza na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda | Azam FC 0-0 Simba SC.

21" Azam wanakosa nafasi nzuri huku wakikosa nafasi kadhaa za kufunga. Hata hivyo umiliki ni upande wao.

25' Simba wanajibu Free Kick ikipigwa na Ndemla lakini golikipa wa Azam anautema na Bocco anapiga tena lakini anakosa.

32' Brayson anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumchezea faulo Bocco, huku Simba wakipata Free Kick amabayo haikuzaa bao.

35' Azam wanakosa nafasi nyingine ya kufunga baada ya mpira kupaa juu. Onyango akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea faulo mchezaji wa Azam.

43' Nado Goooooooooaaal Goooooooaaal. Idd Suleiman anaipatia Azam FC bao la kwanza | Azam FC 1-0 Simba SC.

44' Nafasi kwa Simbaaaaaa... Kagere anapiga kichwa na kutoka nje ya lango la Azam FC ilikuwa nafasi nzuri kusawazisha.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko Dimba la Chamazi Complex ambapo Azam wapo mbele kwa bao moja.

Naaaam mpira ni mapumziko | HT VPL; Azam FC 1-0 Simba SC.

Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Chamazi Complex kwa Kasi ya kama awali huku Simba wakifanya mabadiliko. Ametoka Lwanga na ameingia Nyoni.

50' Kagere anatoa pasi murua lakini Bocco anashindwa kufunga bao, ilikuwa nafasi nzuri ya kusawazisha.

56' Azam wanakosa nafasi ya kufunga ilikuwa movie Kali kuelekea lango la Simba SC.

63' Ametoka Ndemla na ameingia Bwalya upande wa Simba SC.. Umiliki wa mpira ni upande wa Azam.

71' Azam FC wanafanya mabadiliko ametoka Zayd na ameingia Domayo huku Simba wakipata kona ambayo haikuzaa matunda.

73' Ametoka Dilunga na ameingia Mugalu upande wa Simba SC, Simba wanatafuta bao la kusawazisha.

82' Uwanja umeinama upande wa Azam, Simba wanashambulia.

86' Kagere Goooooooooaaal Goooooooaaal

Maddie Kagere wanawarudisha Simba SC kwenye mchezo baada ya shutiiiiii kali kujaa wavuni. | Azam FC 1-1 Simba SC.

90+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo huku Simba wakiwapa wakati mgumu Azam FC

Kwake Bocco anacontrol anapiga shutiiiiii loooooo Nje

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Azam FC wamegawana pointi na Simba SC kwa kufungana bao moja kwa moja. FT, VPL; Azam FC 1-1 Simba SC.

...... Ghazwat....
 
Predictable Simba 11st
Manula
Kapombe
Gadiel
Kenedy
Wawa
Ndemla
Lwanga
Bwalya
Chama
Kondeboy
Bocco
20210715_175439111453.jpg
 
Kwa kuwa Yanga leo imeshinda hivyo hii mechi inakuwa ya burudani tu, Azam hata akishinda hawezi kuzifikia points za Yanga.

Kikosi cha Simba nacho kipo sawa tu tena hata golini leo angepewa nafasi Ally Slim ingekaa poa
 
Back
Top Bottom