Vodacom ni wezi,?

Vodacom ni wezi,?

Emanuel14

Member
Joined
Sep 7, 2013
Posts
32
Reaction score
10
Jamani hawa voda ni wezi, sana leo nimeweka kiasi fulani cha hela ili niweze kujinga na kifurushi, sasa baada tu ya kuingiza vocha salio likasoma sawa sasa ikawa kila ninapojiunga simu, inasema huna salio nikaona niangalie tena salio kwa kuwa sikupiga, na wala sikuandika sms,. Nikaona ni bora niwapigie ili wanipe mchanganuo wa kilicho tokea. Muhudumu aliepokea simu akaniambia nisubiri on line kama dakika mbili hivi baada ya kurudi hewani ananiambia piga simu tena baada ya lisaa limoja. Huku akijua kabisa mida hii ni usiku napia kuwapigia ni gharama. Nashindwa kuwaelewa .
 
wakati mwingine huwa tunajisahau ukishaingiza tarakimu za vocha,tunatupa(imenitokea mara nyingi) karatasi yake bila kuhakikisha kama imeingia ama la.!

Ndio maana hata wewe wakikuomba utaje namba ya vocha ili wahahakishe kama imeingia kwako utaingia kigugumizi tu. !

mhimu tuwe makini pale tunapoweka vocha zetu.
 
Na mimi nimeibiwa hivyo kama mara tatu hivi.Nilikopa salio la sh. 900.Baadae niliingiza vocha ya 1000, wakakata sh.990.Kwa vile nilikuwa kwenye gari na ninahitaji kutumia simu nilikopa papo hapo tena na kupewa sh.900.Nilijaribu kujiunga na kifurushi cha sh.600 lakini voda wakanijibu kuwa sina salio wakati sh.900 nilizokopa sijazitumia.Ikanibidi niweke salio lingine na mkopo wangu ukawa umeliwa.Ni mara tatu nimeibiwa hivi lakini sijapeleka malalamiko kwa sababu ni ngumu sana kupata mawasiliano na wahusika.Voda wajirekebishe vinginevyo tuhamia airtel.
 
Jamani hawa voda ni wezi, sana leo nimeweka kiasi fulani cha hela ili niweze kujinga na kifurushi, sasa baada tu ya kuingiza vocha salio likasoma sawa sasa ikawa kila ninapojiunga simu, inasema huna salio nikaona niangalie tena salio kwa kuwa sikupiga, na wala sikuandika sms,. Nikaona ni bora niwapigie ili wanipe mchanganuo wa kilicho tokea. Muhudumu aliepokea simu akaniambia nisubiri on line kama dakika mbili hivi baada ya kurudi hewani ananiambia piga simu tena baada ya lisaa limoja. Huku akijua kabisa mida hii ni usiku napia kuwapigia ni gharama. Nashindwa kuwaelewa .

Ila ---- hizi smartphone jamani pia tuangalie.nilishakuaga na tatizo kama hilo ikabidi niwafuate pale mlimani city wakaniambia,kwenye smartphone usipojiunga na kifurushi ikiwa bado ni vocha hela inaliwa haraka sana kutokana na automatic update za simu.so chamsingi kabla sijajiunga na kifurushi ni kuzima data kwanza isisome 3G (deactivate data)..ukishanunua kifurushi ndio una allow data 3G..
 
mkuu kwanini usiende polisi kuchukua RB ya wezi wako?
 
Mtandao usio na wahuni ni Airtel tu..!!
mtalalamika mpaka mwisho..
 
.,bosi wao ndo tajiri wa kwanza tanzania kwa wizi kama huu.,.
 
Back
Top Bottom