VODACOM: Mnashawishi watu kununua hisa pasipo kuwapa elimu ya kutosha

peter chula

Senior Member
Jun 8, 2013
123
68
*MAWAZO YANGU LEO*

*VODACOM mnashawishi sana watu kununua hisa pasipo kuwapa elimu ya kutosha juu ya Faida na hasara ya kujiunga na biashara hii, ikumbukwe kuwa hii biashara ni mpya kwa watu wengi ndo maana inakuwa vigumu kufanya maamuzi ya kuzinunua hisa hizo watu wanania, uthubutu na utayari wa kuingia katika biashara hii lakini wanashindwa kufanya maamuzi kwa kukosa elimu hii ya hisa.

Hivyo naona watakaonunua hisa hizi wengi watakuwa waliosoma masomo ya biashara au wenye ufahamu wa kutosha kuhusu biashara hii.

Ombi langu kama Vodacom kweli mnania ya dhati ya kuwasaidia watanzania kuingia katika fursa hii ni vizuri mkatoa elimu kwanza ndo muanze kuuza hizo hisa.

*Naomba kuwasilisha by Peter Chula
 
Back
Top Bottom