Vodacom kweli ni wezi sana comfirmed

Vodacom kweli ni wezi sana comfirmed

Namm nlieweka 2000 vochada huo huo nikacheki Salio ikaja 1664?hata kama ni internet heal yote huyo kwasekunde flani tu.hawa jamaa wezi bana.
 
Vodacom acheni wizi. Binafsi jana nilijiunga na cheka time huwezi amini wakati naongea na mtu ikakata na kuniambia huna salio la kutosha wakati muda wa hiyo cheka ulikuwa haujaisha na nilipocheki salio nikakuta bado muda haujaisha na dakika zipo za kutosha. KAMA CCM NDO IMEWARUHUSU MUWAIBIE WANANCHI ILI WAPATE PESA ZA UCHAGUZI MWAKANI SAWA MAANA SERIKALI YA CCM IPO NA HAISIKII KILIO CHA WANANCHI KUHUSU WIZI WA VODA.
 
Watanzania tusitazamie unafuu katika wizi huu kwani huu ni wizi unaofadhiliwa na serikali yenyewe hii hii ya CCM.
Hao mnaowaita TCRA si lolote ni wala rushwa wakubwa, ------------ kitambo na majambazi hayo yaliyoiweka serikali mifukoni na sasa TCRA wanabaki kuwalamba Vodacom na Tigo makalio ili angalau wagange njaa.
Haiingii kabisa akilini nchi nzima kuwapigia kelele hawa wezi wa Vodacom na Tigo lakini kuwe kimya kama hakuna kitu kinachoendelea.
Hata mimi nimewahi kuibiwa zaidi ya mara kumi na makampuni haya. Kwanza ukiacha salio, asubuhi hulikuti, mwenyewe niliamua kuwahama baada ya kuacha salio la 5,000 na asubuhi kukuta eti salio linasoma Sh. 670/=!
Niliwapigia hawakuniitikia na badala yake kompyuta yao ilinielekeza nikubali kukatwa Sh. 100 ili niunganishwe "haraka" nikiafiki nibonyeze namba 1, baada ya kufanya hivyo niliambiwa " hatuwezi kukuhudumia kwa sasa jaribu baadae" na hela walishakata! Baadae wananambia huna salio la huduma hii! kucheki salio kuna Sh. 40!
Watanzania tuamke; hizi mia mia wanazotuibia ni fedha nyingi sana. Fikiria Voda au Tigo wana kila mmoja wateja milioni Saba, na kati ya wateja hao kila siku milioni nne wanaibiwa Sh. 300/=, makusanyo ya wizi huo yatakuwa zaidi ya Sh. Bilioni moja na laki mbili kwa siku moja na pengine dakika moja! Fedha kiasi hicho inatosha hata kumhonga Rais achilia mbali hawa makuwadi wa TCRA.
Tatizo ni kwamba bado watu wanaendelea kuwapigia kura majambazi hawa katika sare za kijani! Tuna akili kweli sisi?

Wewe ndo huna akili,hivi hata mvua icponyesha utailaumu CCM jinc akili ilivyo mbovu
 
smartphones zinawazingua nyie! Kama unabisha kalalamike TCRA mpaka uone mwisho wake utakuaje, utaumbuka bure. Kama umeliwa na nokia tochi sawa, ila kama una kitu cha android, apple....ujue kazi ni kwako!
 
Hawa jamaa kweli ni 'Wababaishaji' Lakini kuna siku walijichanganya kwenye hiyo Mpesa yao. Nilitumiwa 120,000 baada ya kuitoa nikakaa kama siku 1 kucheki salio tena nakutana na 120,000 from no where kwa kweli sikupoteza muda nilikwenda kuichomoa yote palepale na hadi leo siweki tena pesa kwenye line yangu ya voda wasije wakajilipa.
 
Nimeweka vocha ya elfu2 kucheki Salio mda huo huo nikakuta 1,664 kweli hili kampuni jizi....jihadharini nalo.

Umeangalia kama ulikopa?
Au yamkini kama unatumia internet inawezekana simu yako ilikuwa ina download ukajisahau
Cheki vizuri
 
Jaman jf nilidhan ni mimi tu nawakati mwingine nilidhan makosa ni yangu kweli voda ni wezi mm nimeshanunua line ya baba lao
 
Hivi naomba kuuliza gharama za kuhamisha Pesa kutoka kwenye account ya M-pesa kwenda NMB account ni bei gani?
 
Back
Top Bottom