Vodacom customer care Moshi ni kero

Vodacom customer care Moshi ni kero

CalvinPower

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
1,676
Reaction score
1,061
Vodacom customer care Moshi ni kero.

Nilipotelewa na line yangu ya simu 0755555510 ambayo naitumia kwenye modem. Kifupi siitumii kupiga wala kupokea simu.

Tarehe 13 march nilifaka katika ofisi zao na kujaza fomu kwaajili ya kufanya swap . nilijitahidi kukumbuka namba nilizowahi kuwasiliana na watu nikapata tatu (3) tu. Aliyenihudumia alikuwa kijana mmoja hivi akasema haitawezekana mpaka niwe na namba tano (5) nikamwambia hii line naitumia kwenye modem siitumii kuwasiliana na watu kwahiyo kupata namba tano itakuwa ngumu. Yeye alisimamia msimamo wake na kuniambia nichukue line nyingine. Sikukubaliana nae nikaondoka zangu.

Tarehe 16 march nikapiga simu customer care dar es salaam na aliepokea nikamjulisha yote yaliyonikuta akasema line yangu haina tatizo lolote na nirudi hapo katika ofisi zao zilizopo moshi na kama ikiwezekana nibadilishe mhudumu ili aweze kunisaidia. Nikaingia katika ofisi zao na safari hii nikamfuata mdada mmoja anavaa miwani. Cha kushangaza akachukua form yangu na kwenda kwa Yule aliyenikatalia hapo nyuma. Nafkiri alitaka kujua kwanini Yule kijana alikataa. Wakati na shangashangaa akaja akaniambia hii haifai. KOSA langu ni pale nilipomwambia nimeongea na customer care wa dar es salaam na amesema hii line yangu haina tatizo na nihaki yangu kupata msaada hapa. Basi baada ya kumweleza hivyo akawa mkali na kunirudishia form yangu huku akiangalia monitor yake yaani hata kuniangalia hataki ( jeuri Fulani hivi )
Nikapiga simu customer care dar es salaam wao wakanishauri nionane na meneja. Kwa wakati huo meneja hakuwepo.

Tarehe 17 march ( leo ) nikaamua kwenda Arusha. Wakachukua ile form wakaweka zile namba tatu (3) wakaniuliza line ilipotea lini
nikawajibu kama mwezi hivi. Basi tatizolangu likatatuliwa within 5min.
Nawashukuru sana customer care niliokuwa nawasiliana nao kwenye simu (15366) maana walinitia moyo na wakasema ni haki yangu na nisiache ikapotea. Nawashukuru customer care ofisi za Arusha kwa kunitatulia tatizo langu.
Moshi customer care ichunguzwe na ikiwezekana wapewe mafunzo ya kuhudumia watu bila hasira. Sanasana yule dada mweupe anaevaa miwani.
 
Wamekusikia wakubwa
Wakubwa hao hao ndio wamewaweka pale bila hata kuwapa mafunzo. nafkiri itakuwa mambo ya undugu undugu. Hivi hakunaga chuo ambacho wanatoa mafunzo ya kuhudumia jamii
 
Next time ni PM mkuu dakika tano nyingi hapohapo ulipo nakurudishia laini yako
 
Siku nyingine usikubali kutoka hapo ofisini paka wakupe sababu yenye mashiko kwamba nikwanini hawataki kufanya kazi ilinayowaweka pale. Na ukiwa unauhakika na kile unachokifanya unatakiwa uwe mkali paka wakutekelezee' vinginevyo wasimamishe shughuli zao... Na wakisema umevunja taratibu zao waende wakachukue police. Wanatabia za ajabu sana hao' hasa wakikujudge kama wanavyokudhania wao.
 
Back
Top Bottom