Kuongea na Mhudumu wa Vodacom ni kama imefutwa

maishapopote

JF-Expert Member
May 28, 2009
3,278
5,518
Nina tatizo nimepata kuhusu vodacom sasa nikapiga ile namba yao ya customer care 100 aisee nimeshangaa sana.

Nimehangangaika mpaka nimekata tamaa yaani wamekwepesha makusudi kile kipengele cha kuongea na mhudumu.

Kila kitu kina menu, ndani ya menu yaani utabonyeza moja then tatu then tano haifiki mwisho kabisa wala hamna option ya kuongea na mhudumu, nimekwazika kweli line nimekaa nayo 20 yrs leo nakosa msaada.

Mmekula mkavimbiwa mkajisahau.
 
Hata hao wahudumu huwa wanasaidia basi!!...wahudumu wenyewe sio experts wa telecom, hata vitu basic tu huwa vinawashinda kumuelewa mteja anacholalamika ili kuweza kukiescalate kwa idara husika

Kama una tatizo serious ni vyema ufike Vodashop tu utasaidika zaidi kuliko kuhangaika na wahudumu...
 
Ukiwa unaweka salio la jero jero huwapati ng'ooo au hawapokei simu yako.
Salio la Jero ?

Mi line yangu mkuu ni HPC...hiyo ndio category waliyonipa Vodacom...yaani nikitaka hata kuiswap ni shughuli lazima niende kituo kikubwa...au agent atume email ndio iwe authorised...vocha za hivyo nilitoka mkuu muda sana since 2008...line nimenunua 2004


HPC ni Highly Potential Customer...!
 
Nina tatizo nimepata kuhusu vodacom sasa nikapiga ile namba yao ya customer care 100 aisee nimeshangaa sana

Nimehangangaika mpaka nimekata tamaa yaani wamekwepesha makusudi kile kipengele cha kuongea na mhudumu

Kila kitu kina menu ..ndani ya menu yaani utabonyeza moja then tatu then tano haifiki mwisho kabisa wala hamna option ya kuongea na mhudumu nimekwazika kweli line nimekaa nayo 20 yrs leo nakosa msaada...

Mmekula mkavimbiwa mkajisahau..!


Nafikiri inategemea na mteja, mimi nikipiga, direct inapokelewa. Yani hata si subiri, I think wanapendelea kutokana na matumizi.
 
Mimi nawapata kwa urahisi..

Sehemu nilisumbukaga ni Tanesco, kuna siku simu inaiitaaa mpaka unachoka. Kuna staff wao akaniibia siri, pale pa kuchagua lugha uwe unaweka kingereza.
Jamani ilifanya kazi, simu ndani ya seconds kadhaa ishapokelewa. Na ndio ushakuwa mchezo wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom