Mimi naitumia hiyo ya 10,000 bila kikomo right now, nadhani imetulia sana, unapata 2GB at full speed so kama una kitu cha haraka unataka kushusha unatumia hiyo, then speed inapungua lakini hakuna limit ya kiasi unachoweza shusha so uko limit by speed kwa kifupi.
Nimefanya test ya SpeedTest.Net kwenye simu, wakati ilikuwa bila limit ilikuwa 1430kbps sasa hivi wakati nishapitiliza limit inasema 305Kbps, ni spidi inayotosha kwa kusurf kitu chochote, youtube unaangalia ila inabidi uiruhusu video ishuke kwanza kwa kuweka pause, jana nimeshusha video ya 1.3 GB (torrent) kwa mwendo wa kobe, sio tatizo inabidi uvute subira tu!! Simu inasema nimeshusha zaidi ya 6GB in total hadi sasa.
Natumia Android, narusha Wifi HotSpot nimeunga laptops na tablets, hakuna tatizo. Kwenye simu yenyewe haunotice kuwa ni slow connection, FB, twitter, Mail na website zote zinafunguka fresh. Napata HSDPA (3G) connection hapa nilipo.
Highly Recommended!:majani7: