Vladimir Putin aahidi kutoa siri za mkutano wa Trump na maafisa wa Urusi

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
16,621
30,582
_96087059_9c5c4642-aefa-4ef3-b875-c3aeb0b4ba0e.jpg


Rais wa Urusi Vladimir Putin ameingilia sakata inayomkabili Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na uhusiano wake na Urusi.

Rais Putin amepinga madai ya uvujaji siri za Marekani kwa Urusi na kueleza kuwa yuko tayari kutoa kumbukumbu za mkutano wa viongozi hao kwa bunge na Seneti za Marekani ikihitajika.

Putin ametania hali hiyo na kusema kuwa mkutano haukufanyika unavyodhaniwa.

Majarida mbalimbali ya Marekani yamefichua kuwa Rais Trump aliwapa viongozi wa Urusi taarifa kuhusu Islamic State ambazo zina uwezo wa kuhatarisha watoaji wa taarifa hizo.

Haya yanajiri huku taarifa zikienea kuwa Bw Trump alijaribu kushawishi uchunguzi unaoendelea kuhusu ushirikiano wa wawakilishi wake na Urusi.
Bwana Trump alikutana na waziri wa kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov na Balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak katika ikulu ya White house Jumatano, wiki iliyopita.

Mkutano huo unajiri wakati uchunguzi kuhusika kwa Urusi kwenye uchaguzi wa Marekani unaendeshwa na FBI na kupitia vikao maalum vya bunge za Marekani.

Taarfia hizo zilitajwa kuwa muhimu mno kiasi cha kutoenezwa kwa washirika wa Marekani wakiwemo Urusi wanaoshirikiana na wapinzani wa Marekani nchini Syria.

Hata hivyo Bw Trump alijitetea dhidi ya madai hayo huku mshauri wake usalama wa taifa, HR McMaster akiongeza vitendo vya rais vilikuwa sawa.
chanzo:vyombo vyote vya habari duniani kasoro TBC
 
Hawa mbona wanaongea sanaaaa......kuna kitu kimejificha.Hiyo kitu inawatafuna
 
Hili ni dongo na sasa ni kama imefikia hatua Putin anaiona USA kama kamkoa tu ka Russia. Kwamba White House haiwezi kutoa script au hata tapes za kikao kile? Trump anadharaulika sana
 
Hakuna details alizotoa Trump kwa Lavrov na ndio maana Putin kaingilia kati maana inaonesha Magazeti ya Marekani hayamtaki Trump
 
Mh!, Congress na politicians wa Marekani wanavyomchukulia Putin kwani wataamini basi atakayosema hata kama ya kweli?
 
Wamarekani hawaishiwi ulalamishi,kila siku wanaishu mpya,mara tunatishiwa na kim,hujakaa sawa eti assad anawachoma wafungwa kama viazi ,
sasa kuna siri ipi hapo Trump kuwatahadharisha warusi kuwa ISIS wanapanga kuweka milipuko kwenye laptop na kuingia nayo kwenye ndege?,

tuseme mrusi akiwa na inteligence kuwa newyork kuna bomu la nuclear sehemu litalipuliwa asiwasitue wamarekani eti wafe tu kwakuwa ni maadui?.

Waisrael wanadai eti Trump kawapa warusi siri ya technology yao wanayotumia kuintercept siri za ISIS,
Majigambo tu hakuna cha tech pale,wao waisrael ndo wanawafundisha ISIS namna ya kupack milipuko kwenye laptop kisha wanazunguka na kuleak taarifa kwa marekani ili wapate credit kuwa inteligence yao ni reliable
 
Ukisha kuaa na Rais asie pendwa na wengi mengi huibuka hasa mabaya, tusitegemee kuskia mazuri ya Bwana Trump
 
Back
Top Bottom