Kusherehekea bethi-dei yangu kihenga 26.08 naweka ngoma ya kihenga kama ilivyopigwa na Bana OK chini ya Vieux Papa Lutumba miaka hii ya 20 something katika mtindo wa Rhumba Odemba ya TP OK Jazz. Sikiliza mabinti wanavyokuimbia wakishirikiana na mkaka.
Rhumba ya Bakulutu. Hiyo saxa ndiyo inamaliza mambo. bahati mbaya mabinti waliondoka baada ya Franco kufariki wako ulaya na Oemba International ya Dizzy Mndjeku.
Rhumba ya Bakulutu. Hiyo saxa ndiyo inamaliza mambo. bahati mbaya mabinti waliondoka baada ya Franco kufariki wako ulaya na Oemba International ya Dizzy Mndjeku.
Baada ya Kumsikiliza Vieux Lutumba Simaro, Franco sasa nakuwekea nguli mwingine wa Rhumba Odemba, marehemu Vicky Longomba (Baba yake Awilo na Lovy) hapa akiwa na OK Jazz mwaka 1971 ambao ndiyo wakati aliachana na Franco na kuanzisha bendi yake Orch. Lovy du Zaire. Huyu alikuwa kaka wa Franco (kiumri) na alichangia sana katika kumwonyesha njia za kiutawala kwenye muziki. Co-President wa Band. Ni mwanzilishi wa OK Jazz (1956), Negro Success 1961 na Lovy du Zaire (1971). Ndiyo waimbaji wa kwanza wa OK Jazz-sikiliza sauti yake hapa akisindikizwa na Boyibanda Michaux
.