Viwanja vya mradi Bunju

MKASHU

New Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
3
Reaction score
0
Habari wandugu, kuna kitu kinasikitisha hivi Dar es salaam tena wilaya ya kinondoni hadi leo hakuna umeme ukiuliza utaambiwa wanaleta.

Kuna ndugu yangu anaishi bunju kwenye maeneo ya bunju kulikokuwa na mradi hadi leo hakuna umeme na sasa hivi wameanza kusambaza nguzo lakini kama wewe hujulikani basi utaendelea kukaa giza mpaka tanesco wafurahi ndio utaona umeme hatujui ni lini.

Embu tujiulize kweli kuna haki kweli wakati huduma yenyewe utakuja kuilipia na kuiingizia nchi yetu mapato?
 

Si walitandika line kubwa zimebaki tu zile za kuvuta kuingia majumbani?
 
Bunju huko huko hata mradi wa maji ya wachina wameuchakachua
 
Hata kama wakitandika nguzo, nyaya hadi mita au luku, huo umeme uko wapi?? Sisi tuna mita na luku lkn umeme uko wapi, hela ninayo lakini hiuo umeme uko wapi!
 
Bunju huko huko hata mradi wa maji ya wachina wameuchakachua

Waulize Kijitonyama mitaa ya Heko habari ya maji ya wachina, mabomba yalipitishwa yalipokamilika hakuna maji wala wachina wahakurudi kusema kulikoni. Mafisadi wa maji wameungana na wananchi walafi wakachimba visima kisha wakakata mabomba yanayokwenda kwa raia wengine. Cha kushangaza unakuta mtaa mzima hauna maji, wenye maji ni ya visima tena ya chumvi, kuna bwana mmoja anaitwa Liundi anauza maji safi, sasa jiulize hayo maji yeye anatoa wapi? Wateja wake ni wafanyabiashara wadogo wadogo hadi wale wenye magari ya maji pale Science.

Ukienda Dawasco na kuwakali akooni na ushahidi kibao wako, wanakwenda pale danganya toto, mabomba yanafungwa maji yanatoka mtaa mzima, siku mbili tatu hali imerudi pale pale.
 
we tafuta njia mbadala hata hao wenye umeme wanamgao, afadhali uwe na umeme wako kuliko kutegemea wa TANESCO
 
wahusika ukiwafuata wanasemaje?hapo ndipo pa kuanziaaa
 

Pole sana......ila usijali kwakuwa wenzio tuna mgao
 
Hata kama ukifungiwa umeme na mgao huu utajsikia tu hauna umeme
 
Hii ndio Tanzania zaidi ya unavyoijua! Sio Bunju tu bali kila walipopima viwanja ni utapeli kwa kwenda mbela! Subiri uone kitakachotokea KIGAMBONI ambako wanadai utakuwa mji wa kisasa kama hujakuta hata barabara moja hamna1 luguruni walituonyesha utakuwa mji wa kisasa lakini leo hii ni vichaka vitupu! Ndugu zangu wa Kigamboni nawaasa msikubali hilo dudu linaloitwa KIGAMBONI BLUE DIAMOND1 mtanyag'anywa maeneo yenu halafu wote mnaenda kulundikwa kijisehemu kimoja kama kuku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…