Viwanja kushuka bei Mwakani

brightoscar

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
369
541
Jinsi uchumi wa nchi unavyoenda kwasasa mpaka kufika mwakani bei za viwanja zitapungua kwa asilimia kubwa.

Watu waliokuwa wakiingia ofisini kwa siku anatoka ametengeneza milioni 3 hawapo tena hawa ndio waliokuwa wanasababisha viwanja kupanda bei maana hata akiambiwa milioni 100 hawazi.

Ukosefu wa fedha kwa watu wengi baada ya kufutwa kwa seminars na safari zilizokuwa hazina mpangilio wengi sasa wanategemea mshahara hili litasababisha kuanza kuuza asset walizokuwa nazo kama mtu alikuwa na viwanja vinne atataka auze viwili ili awe na uwezo wa kuviendeleza viwili vilivyobaki.

Maisha yatakuwa tofauti sana mpaka kufikia mwakani mifumuko ya bei iliyokuwa inatengenezwa na wafujaji wachache inakwenda kuisha wekeni akiba itawasaidia muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom