Viwanja Kigamboni Mwasonga Milioni 1 tu kwa heka.

Viwanja Kigamboni Mwasonga Milioni 1 tu kwa heka.

Gazillionaire

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2013
Posts
235
Reaction score
59
Habari gani wakuu? Nimewaletea habari njema!
Nauza viwanja KIgamboni eneo la Mwasonga ambalo liko baada ya Dsm Zoo.
Eneo ni zuri sana, maji yako karibu, panafaa kwa ufugaji wa samaki, kuku, Ng'ombe, mbuzi, na wanyama wengine kwani hakuna milipuko ya magonjwa wala mbung'o wanaodhuru ng'ombe.
Pia eneo linafaa kwa kilimo cha matikiti, Bamia, viazi vitamu, mchicha na mboga nyingine za kibiashara.
Eneo lilipo pana miradi miwili mikubwa ya ujenzi wa makazi ya watu ambayo iko chini ya vyama vya ushirika(Saccos) , Mradi wa maji wa Dawasco ambao wamechimba zaidi ya visima vinane vya kisasa vyenye kina kwa ajili ya kusambaza maji kwa wakazi wa maeneo hayo na yote yaliyo karibu.
Eneo liko mbali na mradi wa mji mpya wa kigamboni na haliko kwenye utaratibu wa mradi huo wala mwingine wowote kwa hiyo ni salama kwa uwekezaji na makazi pia.
Bei ya heka moja ni sh. 1000,000/= .
Karibuni Mchangamkie fursa hii! Piga 0686555726
 
Maji yapo karibu unamaanisha nini, kuna mto?, hayo maji ya visima ya Dawasco hayana chumvi?
 
Asante, ni kilomita ngapi kutoka ferry na kutoka daraja mpya inayojengwa? Una eneo kubwa kiasi gani. Umbali toka beach ili tujue hivyo visima vitafaa matumizi gani.
 
Maji yapo karibu unamaanisha nini, kuna mto?, hayo maji ya visima ya Dawasco hayana chumvi?

Ni Kina cha kwenda chini pale utakapoamua kuchimba kisima cha maji.
Visima walivyochimba Dawasco ni vile vikubwa ambavyo vina uwezo wa kunywesha miji, hawajaanza bado kusupply lakini kawaida maji yao yanakuwa treated kuondoa chumvi kwa hiyo huwezi kujua kuwa kule yalikotoka yalikuwa na chumvi au lah. Hata hivyo maeneo hayo hayana maji yenye chumvi ingawa ni km 6 mpaka 8 kutoka baharini.
 
Hakuna utata wowote, labda ungefafanua Mkuu.

1. Vipo umbali gani kutoka barabara kuu ya kwenda mwasonga?

2. Sehemu vilipo Unaipita njia panda ya kwenda kimbiji?


Maisha ni kama kioo,ukicheka na yenyewe yanacheka
 
Asante, ni kilomita ngapi
kutoka ferry na kutoka daraja mpya inayojengwa? Una eneo kubwa kiasi
gani. Umbali toka beach ili tujue hivyo visima vitafaa matumizi
gani.

Ni km kama 25 mpaka 28 kutoka ferry, Km kama 22 mpaka 24 kutoka Daraja jipya.
 
Mil. 1 kwa heka bei nafuu. Hakuna matatizo kweli? Isije tukanunua viwanja kwenye eneo la mradi wa Sirikali ikala kwetu!
 
Kwa daresala ni nani anayeweza kuuza kiwanja kwa milion moja tuu

hili ni km tangazo la kujiunga na DECI
 
Mil. 1 kwa heka bei
nafuu. Hakuna matatizo kweli? Isije tukanunua viwanja kwenye eneo la
mradi wa Sirikali ikala kwetu!

Hakuna tatizo hata moja, mradi haufiki Mwasonga, uliza mtu yeyote anaeijua kigamboni atakwambia nachokisema.
 
Kwa daresala ni nani anayeweza kuuza kiwanja kwa milion moja tuu

hili ni km tangazo la kujiunga na DECI

Kuna ndugu yangu aliwahi kuweka thread humu ya viwanja maeneo hayo kwa milioni 2.5 kwa heka, watu wakapiga kelele wapunguziwe.
Viwanja mwasonga bei iko juu ni kweli, ni shida ya kutatua mambo tu ndio iliyofanya leo ukute viwanja vya bei hii kwa maeneo ya huku kuna faida gani ya kuandika bei kubwa ukaishia kutazama namba tu ulizoandika bila kupata mteja?
Lakini vikiuzwa viwili vitatu, matatizo yakatatuliwa inawezekana nikabadili mawazo na bei ikarudi pale ulipopazoea.
 
Sawa lkn kumbuka heka moja ni kubwa sana

hapo mafisad na mapedeshee wakisikia hizi habar watanunua hadi nyasi km ni kweli
 
samahani, najua sio mahala pake. Ila naomba kuuliza anayepajua Marogoro,huko huko kgamboni.

kuna kiwanja,sema nina maswali khs umbali etc
 
samahani, najua sio mahala pake. Ila naomba kuuliza anayepajua Marogoro,huko huko kgamboni.

kuna kiwanja,sema nina maswali khs umbali etc

Marogoro ni kama km 45 kutoka ferry, ni mbele ya Mwasonga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom