broken ages
JF-Expert Member
- Mar 23, 2012
- 235
- 84
Mheshimiwa Rais Magufuli amefanya jambo bora na la msingi sana kupiga marafuku uagizaji wa sukari toka nje ya nchi hili ni jambo bora na la msingi sana kwa ustawi wa taifa letu,
Jambo ambalo tawala zilizomtangulia na hasa utawala aliourithi ulishindwa kufanya pengine ilikuwa ni kwasababu ya kuyalinda maslahi ya wachache ama ni utashi wa kushindwa kuliona jambo hili,
Hili linatupa ujumbe wa ni kwa namna gani Rais Magufuli alivyokuwa hana makundi anayoyalinda kwa manufaa yao binafsi ndani ya nchi hii
Faida ya kuzuia uagizaji sukari toka nje ni nyingi lakini kubwa sana ni kutoa nafasi kwa viwanda vya sukari Tanzania kufanya kazi kwa ufanisi na tena kuongeza tija kwa kupata fursa ya kufanya kazi na hata kuongeza ajira kwa watanzania kwani kwa namna hii viwanda vya sukari vitaongezeka kwasababu vitakuwa vikifanya kazi kwa faida.
Hapa ningemwomba mheshimiwa Rais kupitia idara zinazohusika kutoa pia ushauri Kama siyo kuwaelekeza wazalishaji wa sukari namna bora na nzuri ya kusambaza sukari hadi kumfikia mtumiaji wa mwisho kwa bei nzuri
Nasema hivi kwa sababu kunao ukiritimba mkubwa sana kwa namna ya kuipata sukari kutoka viwandani na hasa TPC Moshi, kwani kiwanda kimewaweka ama kuteua wafanya biashara wachache kuwa ndo wanaowaruhusu kununua sukari kutoka kiwandani, kwa mfano kwa mikoa kama Kilimanjaro na Arusha utapata kuwa ni wafanyabiashara watatu ama wanne wanaoruhusiwa kununua bidhaa hii adimu ya sukari kutoka kiwandani na hii nionavyo mimi madhara yake ni makubwa kwani hawa wafanyabiashara wachache na tena katika hao nusu yao wakiwa si wazawa ni rahisi kufanya makubaliano na wakauza sukari kwa bei wanavyotaka wenyewe.
Kwani kwa hapo uhuru wa soko haupo ni tofauti na kwamba ingekuwa kila mfanyabiasha mwenye uwezo na aruhusiwe kununua jambo ambalo lingetoa nafasi nzuri ya ushindani wa kweli katika soko sioni kama kuna sababu gani ya kuwatunukia watu wachache nafasi hii adimu ya kusambaza sukari,sioni ni kwa nini isitolewe nafasi kwa wafanyabiashara wengi kama siyo wote kuingia kiwandani na kupatiwa bidhaa kwa bei ya kiwandani ili wakashindane kuuza kwenye masoko.
Ikifanyika hivi itamwondoa hata mheshimiwa Rais lawamani kwani hakutakuwepo upandishwaji bei kiholela na hivyo bei kubakia kuwa chini kukaribia kama siyo sawa na ile sukari ya nje ambayo haitakuwepo tena madukani.
Namwomba Rais ama waziri mwenye mamlaka ingilia hili ili kuundoa ukiritimba uliopo Tpc na ambao hauna tija kwa wengi ila unao maslahi makubwa sana kwa wachache.