Viwanda vya sukari fungueni vituo vyenu wenyewe vya mauzo

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,994
Nchi hii kuna wafanyabiashara wa jumla ambao kazi yao ni kuhujumu viwanda vya ndani na kutegeneza upungufu wa bidhaa usiokuwepo ili wapandishe bei na kuua viwanda vyetu ili waagize bidhaa nje ya nchi toka viwanda vya nje ambavyo huwahonga wafanyabiashara hao pesa nyingi ili wahujumu viwanda vya ndani wauze bidhaa zao.

Kuna rushwa za kimataifa ambapo wafanyabiashara wa nje huhonga wafanyabiashara wakubwa wa ndani ili waue viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa zinzazofanana na zao.

Dawa ya viwanda vya ndani kutokufa au kuuawa na wafanyabiashara wakubwa wanatakiwa wafungue vituo vyao wenyewe vya mauzo au wasambaze moja kwa moja kwa wafanyabiashara wadogo (RETAILERS).

Wawe na magari yao na mabohari yao mikoa mbali mbali ambako watapeleka bidhaa zao kama sukari na kuanza kusambaza wenyewe kwenye kwenye maduka na taasisi.Wauze direct kwa retailers kama ambavyo Cocacola,AZAM nk wanavyofanya.

yehodaya123@gmail.com
 
Back
Top Bottom