mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,172
- 1,074
Kumekuwepo na vizingiti kadhaa katika uanzishaji wa biashara mpya {kodi za awali} na uwekezaji wa viwanda hasa unaohusisha upatikanaji wa hati ya mazingira {Environmental Impact Assessment- EIA}.Kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu tukufu mwekezaji wa ndani ama wa nje hawezi kuwekeza ama kufanya ujenzi wa miundombinu mpaka tathmini ya athari za mazingira zimefanyika.
Mchakato wa upembuzi yakinifu huchukua muda na kugharimu fedha nyingi sana,Mathalani yaweza kumgharimu mwekezaji mpaka 50,000,000 au kuzidi.Wakati haya yakifanyika mwekezaji bado anakuwa hana uhakika wa kufanya uwekezaji wake mpaka hati ipatikane toka NEMC.Baadhi ya maafisa wa NEMC ni kama miungu watu,nenda rudi,nenda rudi,masahihisho yanayozidi thesis ya mtahiniwa wa shahada ya uzamivu.Inasemekana katika michakato mingi bila mlungula kutolewa cheti husika chaweza kuchukua miaka.
KIINI CHA KERO:
Nchi ina kiu ya kupata uwekezaji mkubwa na mdogo,nchi ina kiu ya ajira kwa vijana walio wengi kutokuwa na kazi katika taifa..Nchi inahitaji fedha kwa ajili ya kugharamia utoaji wa huduma za kimsingi kwa wananchi {afya,maji,umeme,barabara,n.k}.
Ipo miradi mingi imekwama sababu tu ya michakato yenye urasimu ya utoaji vyeti vya athari za mazingira toka NEMC..Ni kweli mazingira ni uhai lakini je kwa kiwango gani tathmini husika zinazingatia uzalendo,ukweli,weredi katika utunzaji wa mazingira sehemu nyingi za nchi yetu {utiririshaji wa maji yenye sumu toka katika Migodi,viwanda n.k}.
Wito:
Watendaji wa taasisi za umma wanapaswa kutenda kazi na kutekeleza wajibu wao kwa kutanguliza maslahi mapana ya taifa na sio maslahi binafsi.Vivo hivyo wataalamu washauri katika nyanja nyeti na za kimkakati wafanyiwe auditing za kimaadili ili kuwafanya watekeleze majukumu yao kwa wakati,weredi na viwango {Uzalendo,Uadirifu,umakini}.Ipo haja pia ya kutathmini shughuri zenye usumbufu kwa wawekezaji zinazofanywa na baadhi ya taasisi kwa wawekezaji wenye viwanda kama zifanywazo na OSHA,WCF,MUNICIPALS,TBS,FIRE,N.K