VItuku vya Kura za maoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VItuku vya Kura za maoni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by BornTown, Aug 5, 2010.

 1. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kura zachomwa moto Singida


  [​IMG]Thursday, 05 August 2010 06:30
  Na Kitiko Mpacha, Singida
  JESHI la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu wanne wakazi wa Kijiji cha Iglansoni Kata ya Muhintiri wilayani Singida, kwa tuhuma ya kuvamia Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupora kisanduku cha kura za maoni kisha kuziteketeza kwa moto.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Bi. Celina Kaluba, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti Mosi mwaka huu saa 12.30 jioni katika kijiji cha Iglansoni.

  Kamanda Kaluba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bw. Shambuli Shija (44), Bw. Manyanda Lazima (46), Bw. Clement Richard (36) na Bw. George Petro (38).
  Alisema siku ya tukio watu kadhaa waliokuwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni za CCM za udiwani na ubunge walivamia ofisi za chama hicho kijijini hapo na kupora kisanduku cha kura na kwenda kuzichoma moto.
  Alisema wakati kundi hilo la watu wakifanya vurugu hizo, hapakuwa na ulinzi wa kutosha wa askari polisi na kwamba mgambo wa kijiji pamoja na sungusungu waliokuwa wakifanya ulinzi walishindwa kuzuia vurugu hizo.
  "Ni kweli hapakuwa na askari polisi, hatuwezi kuenea wote ikizingatiwa kuwa pia kuna upungufu wa vitendea kazi kama vile magari. Hatukuweza kusambaza askari wetu maeneo yote, Iglansoni ni mbali sana karibu kilomita 150 kutoka hapa mjini," alisema Kamanda Kaluba.
  Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu hao walitenda kosa hilo kwa madhumuni ya kuvuruga matokeo ya kura za maoni baada ya kutokea mchuano mkali baina ya wagombea wawili wa nafasi ya ubunge.
  Matokea ya kura za maoni katika jimbo hilo bado ni kitendewili kutokana na kura kuendelea kuhesabiwa huku katibu wa CCM Singida Vijinini, Bw. Cosmas Kasangani, akiahidi kwamba yatatolewa muda wowote.
   
Loading...