Vituko vya tume ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya tume ya uchaguzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUKUTUKU, Oct 29, 2010.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nimepatwa na mshangao na utendaji wa tume ya uchaguzi,nilikwenda kuhakiki jina langu kwenye kituo ambacho nilijiandikisha,lakini kwa bahati mbaya sikuliona jina langu katika orodha ya wapiga kura halali.Baada ya kuona hivyo nilijalibu kupiga simu namba “+255222199780” ambayo ilitolewa na tume ya uchaguzi ili kujibu maswali ya wapiga kura wenye matatizo,nilipoipiga namba hii waliniambia niwatajie namba ya kadi yangu ya mpiga kura .Baada ya hapo wakaniambia inavyoonekana simo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.Pia wakanishauri nitume namba yangu ya kitambulisho cha mpiga kura kwenda “15455” na nilijibiwa “Ombi lako halikufanikiwa,tafadhali hakikisha namba yako ya utambulisho wa kupiga kura kasha tuma tena baadaye”.Baada ya hapo, wakanishauri niende posta house Gorofa ya saba ambapo ofisi ya tume uchaguzi ilipo,nikaenda kufika huko wakaniambia niende bohari,kabla sijaondoka wakabadilisha tena na kunishauri niende kwa katibu mtendaji wa kata.Sikuchoka,nikaenda kufika huko,yeye akaniambia “sasa kama haupo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura unataka nifanye nini?mimi sina uweze wa kuongeza au kupunguza jina nakushauri uwende kwa mkurugenzi wa halmashauri,ambaye ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika eneo hili”
  Sasa mimi nimeshakata tamaa kabisa kwa kuwa inavyoonekana tume ya uchaguzi hawakufanya maandalizi yoyote ya namna ya kushughulikia matatizo ya wapiga kura na hawajui wanachokifanaya,kama wanajua basi wana dhamira mbaya.Walitakiwa wawe na mpangilio maalumu wa kushughulikia matatizo ya wapiga kura.Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu.Naomba ushauri wenu ili niweze kupiga kura na kuchagua kiongozi bora.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waache usanii watoe ushirikiano kwa wataka mabadiliko.
   
 3. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Wenye matatizo kama haya ni wengi tu. tatizo langu mimi ni kwamba wamekosea kuspell jina langu nimekwnda mpaka kwa mkurugenzi wa halmashauri na akaniambia hamna shida its just a human error na nitapiga kura bila wasiwasi. sijui kama ni longolongo au ntafika pale na kurudishwa?
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Na mimi nitajalibu kwenda kwa mkurugenzi wa halmashauri nimsikie atasemaje!!!
   
 5. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Leo ndo siku pekee iliyosalia, Tutakosa kura yako mkuu, nenda chap.
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama utakua umeongea kwa lafudhi ya kinyumbani wameshajua kura yako utampa nani ndio maana wamekubania.........
   
Loading...