Vituko vya abunuasi ni noma

Vituko vya abunuasi ni noma

Ile kali zaidi ya Abunuwasi ni pale alipokuwa na shida na Sultani. Kufika mlangoni kwa sultani wale mlinzi akakataa kumruhusu aingie kumwona. Abunuwasi akaomba sana aruhusiwe kumwona Sultani maana alikuwa na shida kubwa. Mlinzii alijuwa kuwa abunuwasi akiingia kwa sulatani atapata anachotaka maana alipendwa sana na sultani. Mkwara aliompa ni kwamba aahidi kuwa atakachopata kwa sultani wagawane nusu kwa nusu na mlinzi wa sultani, abunuwasi akakubali na akaingia kwa sultani. Kufika ndani sulatani anamuuliza sema shida yako abunuwasi maaana leo unaonyesha una huzuni. Abunawasi akasema Seyidina wangu naomba unichape viboko mia, Sultani akashangaa, kwa kosa gani? Abunuwasi akasema nichape tu Seyidina wangu na akasisitiza kuwa haondoki mpaka achapwe. Sulatani akaamura askari pale kwenye kiti cha enzi amtandike Abunuwasi taratibu sana viboko mia. Walipomchapa mpaka viboko hamsini Abunuwasi akasema vimetosha maana mlinzi wa pale getini tumekubaliana kuwa nitakachopata humu ndani kwa sultani lazima na yeye apate nusu yake kwa hiyo hivyo hamsini vilivyobaki atandikwe mlinzi. Sulatani kusikia hivyo akaghadhabika sana na kuamuru mlinzi aletew apigwe viboko hamsini tena vya uhakika. Mlinzi alijuta kuzaliwa, na hakurudia tena kuomba rushwa
<br />
<br />
Duh Mkuu umenifurahisha sana. Abunuwas mwisho.
 
vitabu vile nitavipata wapi wana jf?hakuna website yenye hadithi zile?

kama sikosei kampuni ya mkuki na nyota ya walter bgoya inachapisha vitabu vya zamani. nimeviona vya alfu lela ulela sina na vya abunuwasi kavichapisha.
 
Kali nyingine ya Abunuwasi ni yule masikini aloyetowelea chakula chake na harufu nzuri ya samaki aliekuwa anapikwa nyumbani kwa tajiri. Kesho yake akakutana na yule tajiri na kuanza kumshukuru kuwa alifaidi sana chakula chake kwa harufu ya samaki kutoka nyumabni kwake.

Yule tajiri alisikitika sana na kukasirika kuwa ndio maaana samaki yule hakuwa na ladha sababu ya masikini yule kuvuta harufu yote ya samaki, hivyo alimwambia amlipe reale 5 kama fidia. Masik8ni yule fedha hiyom hakuwa nayo. Akaenda kushtaki kwa Sultan Harun Rashid ambaye naye alimkandamiza kuwa lazima alipe.

Mmasikini akaona aende kwa Abunuwasi kupata ushauri. Abunuwasi akamwambia yule masikini kuwa atamlipia deni hilo ila mbele ya Sultani. Siku ya kulipa Abunuwasi akaenda na hizo reale tano kwa sultani ili alipe deni hilo.

Wakati anataka kumpa yule anayedai abunuwasi akadondosha zile fedha sakafuni na kisha akamwabia yule tajiri kwa Chukua huo mlio kama malipo maana na yeye masikini alikula harufu tu.
 
hiyo kali, nimetamani mambo ya Abunuwas, natamani vitabu vipatikane madukani kama vitabu vya Nyangwine
 
Kali nyingine ya Abunuwasi ni yule masikini aloyetowelea chakula chake na harufu nzuri ya samaki aliekuwa anapikwa nyumbani kwa tajiri. Kesho yake akakutana na yule tajiri na kuanza kumshukuru kuwa alifaidi sana chakula chake kwa harufu ya samaki kutoka nyumabni kwake.

Yule tajiri alisikitika sana na kukasirika kuwa ndio maaana samaki yule hakuwa na ladha sababu ya masikini yule kuvuta harufu yote ya samaki, hivyo alimwambia amlipe reale 5 kama fidia. Masik8ni yule fedha hiyom hakuwa nayo. Akaenda kushtaki kwa Sultan Harun Rashid ambaye naye alimkandamiza kuwa lazima alipe.

Mmasikini akaona aende kwa Abunuwasi kupata ushauri. Abunuwasi akamwambia yule masikini kuwa atamlipia deni hilo ila mbele ya Sultani. Siku ya kulipa Abunuwasi akaenda na hizo reale tano kwa sultani ili alipe deni hilo.

Wakati anataka kumpa yule anayedai abunuwasi akadondosha zile fedha sakafuni na kisha akamwabia yule tajiri kwa Chukua huo mlio kama malipo maana na yeye masikini alikula harufu tu.

Nimependa akili aliyoitumia abunuasi hapo
 
Abunuwas was the great...zipo nyingi sana hadithi zake na zilikuwa na mafunzo kweli...
Kuna moja abunuwas nyumba yake iliungua moto,akifikiria atafanyaje na yale majivu ya nyumba yake akapata jibu,akayapakia magunia kibao ya majivu kwenye punda akafanya safari ya kwenda nchi ya mbali, kufika kule alikuwa na gunia moja lililokuwa na sugari.Akatangazia mji ule kuwa amekuja na biashara ya sukari nzuri sana...wakuu wa mji ule wakapikiwa chai yenye sukari wakaipenda sana.Abunuwas akafanya biashara nzuri ya kuuza na yale magunia yote ya majivu nakurejea kijiji kwake akiwa na ukwasi mkubwa wa fedha....
Wanakijiji wakajiuliza huyu bwana imekuwaje kaondoka na yale majivu ya nyumba yake iliyoungua na kurejea na mihela mingi?!...wakajiongeza wenyewe kwa kuchoma majumba yao na miti ili wapate majivu mengi kwenda kufanya biashara alipotokea Abunuwasi...
kilichotokea huko nitamalizia baadae!
 
kuna ile alienda kuazima sufuria 2 akarudisha 2 mwenye vyombo alivyouliza asema zimezaa baadae akaenda kuazima tena sufuria 5 hakurudishs mwenye vyombo allvyo fuata akaambiwa vimekufa!
 
Nazikumbuka saaana enzi hizo....maadili yalikuwepo sio zama hizi eti digital kumbe sio ishu wala nini!
 
abunusi alikuwa na ghorofa lake,sasa alipoona maisha magumu akauza vyumba vyote vya juu yeye akabaki na vyumba vya chini, cku akiishiwa hela anatangaza hiv, jamani eee mimi nabomoa nyumba yangu ya chini nyie wa juu tafuteni mahali pengine mkakae, basi wanamlipa hela ili asibomoe
 
Back
Top Bottom