Vituko mitandaoni. Tupia chako

MUHIMU```
Kuna siku marafiki tutatengana
hatutaonana tena wala kuwasiliana.


Wengine umri utakuwa umeenda
sana wamekuwa wazee na wengine hawatakuwepo duniani.


Tutakumbuka
tulivyokuwa tunachat
tutakumbuka tulivyokuwa tunapendana
na kushirikiana
tutakumbuka tulivyokuwa vijana wenye nguvu
tukikimbizana
huku na kule lkn hatutaweza kuwa pmj tena.


Labda bado tutakuwa na picha
za marafik zetu tutaziangalia na kukumbuka mengi.


Watoto na wajukuu zetu watatuuliza
"Ni kina nani hawa
?"

Kwa maskitiko tutawaambia "Ni wapendwa wetu tulioshirikiana na kupendana nao"


Huzuni zitatufunika maana hakutakuwa na njia ya kuonana tena zaidi ya kukumbuka enzi zetu!


Huu ni wakati wa kufurahi na marafiki
na kutendeana mema ili tusije kujuta baadae.


Huu ni wakati wa kupendana na kila aliye karibu na wewe.


Onyesha upendo
na moyo
wa furaha kwa kila unaechat nae kwa sasa.


Tunza kumbukumbu za yale mazuri unayotendewa na marafiki zako


Tunza picha zake kwa bidii


Kama unakubaliana na mimi wakumbushe marafiki zako wote kuwa upendo
ni kitu cha thamani sana!!


Mkumbushe kila unayechati naye kuwa hataendelea kuchat na wewe milele hivyo autumie huu wakati
vizuri.


Kama na mimi ni mmojawapo nikumbushe kukuthamini na kukutendea mema


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…