Vituko mitandaoni. Tupia chako

Price tag ya milioni 20 imepata matumizi mengine kwenye shopping za Tanzania baada ya Duka maarufu la vifaa vya majumbani la ABC Emporio Dar es salaam kuonesha choo kipya cha kukaa kinachouzwa kwa shilingi milioni 20 za Kitanzania.

Ni choo ambacho kinampa Mtumiaji massage wakati anapokitumia, kinamtawaza, kumpa joto kama anahisi baridi pamoja na huduma nyinginezo ambazo Mtumiaji anaweza kuzichagua kwa kutumia rimoti maalum inayokuja na choo hicho.

Meneja Masoko wa Emperio Rashid Ally amemwambia Mwandishi wa @AyoTV_ Paschal Mwakyoma kuwa tayari vyoo vya aina hii visivyopungua vitano vimeshanunuliwa, video nzima kuhusu choo hiki ipo hapa youtu.be/zH-tDsKJyY8

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…