Unafanya kazi serikalini, mshahara wako ni shilingi laki 8. Huna biashara nyingine ye yote lakini kwa mshahara huo huo unamiliki viwanja Mbweni na Kigamboni, unajenga maghorofa Sinza na Tabata, umenunua V8, unasomesha watoto Uchina na Uturuki. Hukuachiwa urithi wo wote na wazazi hivyo anayejua unapataje pesa hizo ni Mungu pekee anayejua na genge unalotumika pamoja nalo. Unawasaidia katika kupora, wewe unabaki na chenji (Amos 5:11).