Kifo kinatisha...
Kifo kinaogopesha...
Kifo hakizoeleki....
Kuna mwaka nilikuwa nauguza mgonjwa hospitali ya Muhimbili, nilikuwa nashinda pale siku nzima naondoka saa tano au sota usiku kila siku....
Nilikonda haswa.
Hilo gari/machela inayobeba maiti kutoka wodini kwenda mochuari ni ya bati sasa ikiwa inatembezwa kwenye zile korido, unajua tuu tayari kjna mtu kesharudosha namba.
Ilikuwa inanipa taswira na fikra mbaya kila nikisikia muungurumo wa matairi wa machela ya bati.....
Sijui kwanini hawabuni namna ya kubeba marehemu kimya kimya kwa namna ambayo kama my haangalii hawezi jua kama maiti inapelekwa mochuari.....
.