Hicho ndicho kitakachokupata, kwa mfano, ukija kwangu Misungwi. Utachinjiwa beberu la mbuzi na matokeo yake ndo hayo. Nyama za kila aina. Na ni lazima ule kweli kweli maana usipokula ni dalili ya dharau na kutukosea heshima wenyeji wako. Na nyama zingine zinakaushwa (mitanda) ukiondoka tunakubebesha. Ikibidi na ngozi ya beberu lako pia unafungiwa vizuri.