MFANYAKAZI ili Afukuzwe Kazi Kwa Sababu ya UTORO/KUTOKWEPO KAZINI, Inatakiwa Asiwepo Kazini Kwa
Zaidi ya Siku Tano (5) za Kazi Bila Ruhusu au Sababu ya Msingi.
Wazee wa Mahakama ya Rufani Wamekubali Kupitia (Review) Upya Maamuzi Yao, Watoto wa Mjini Wanakwambia: Wazee Wamekubali Kuyarudia Matapishi Yao.
Iko Hivi,
25/9/2009 COSTANTINE Alifutwa Kazi na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Sababu ya Kutokwepo Kazini. Akafungua Kesi Kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Akashinda, CMA Iliamuru
Arudishwe Kazini na Alipwe Mishahara Yote Ambayo Hakulipwa Tangu Kufutwa Kazi.
Muhimbili Wakaenda Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi,
Wakashindwa, Wakaenda
Mahakama ya Rufani (Revision),
Wakashinda Hiyo ilikuwa
29/01/2016, Mahakama ya Rufani Ilitengua Maamuzi ya Mahakama za Chini,
ilisema Alifutwa Kazi Kihalali, Ilionekana HAKWEPO KAZINI KWA SIKU SABA (7).
Sasa CONSTANTINE Akawarudia Tena Wazee wa Mahakama ya Rufani ili Wayapitie (Review) Upya Maamuzi Yao,
Imekuja Kuonekana Katika Zile Siku Saba (7) Ambazo ilionekana Hakwepo Kazini, Siku Zingine Zilikuwa Weekend na Sikukuu ya Idi,
Hazikuwa Siku za Kazi, Kwahiyo Baada ya Kuziweka Pembeni Hizo Siku,
Imegundulika HAKWEPO KAZINI KWA SIKU NNE (4) TU na Sio Siku Saba(7). Kanuni za Kazi Zinasema Ili Afutwe Kazi
Inatakiwa Asiwepo Kazini Kwa Zaidi ya Siku Tano (5).
Hivyo,
24/10/2022 Wazee Wameunga Mkono Maamuzi ya CMA na Mahakama Kuu, Alifutwa Kazi Kimakosa. Sasa
Tupo 2022,
Alifutwa Kazi 2009, Kwahiyo
Atarudishwa Kazini na Kulipwa Mishara Yote Kuanzia
2009 Mpaka 2022!
Hii ni Moja ya Kesi Adimu Sana, Wazee wa Rufani Wanakubali Kureview Maamuzi Yao. Ikae Kabatini.
MD, Mendez (M.C.A)