Mkwara wa babu
Mzee mmoja alipanda Gari Stend;
Wakati wa kugombania Siti,
Akaibiwa Nauli.
Akasimama katikati ya Gari-Akatangaza; “Jamani Naomba Aliyeniibia Pesa yangu Arudishe Haraka,
Tena Fasta kabla Sijafanya Tukio kama Nililofanya 1977″
Abiria kuskia hivyo wakaogopa.
Ikabidi Mwizi Ajitokeze,
Akarudisha Pesa na kuomba msamaha!
Abiria mmoja akauliza:: Mzee, Kwani 1977 Ulifanya tukio gani?
Babu: Si nilienda kwa Miguu mpaka Nyumbani!