Mjini shule..
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea.
Baada ya wiki nampigia simu hapokei, nimempigia zaidi ya mara 10 kimyaa!
Nikaona isiwe shida nikamwandikia message kwa WhatsApp:
"Hello Mum, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba N). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama hana akili nzuri.."
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu mfululizo kama mara 20, mie kimyaa..
Akatuma message:
"Hao wanawake unawajuwa, β¦mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliβ¦!"
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaβ¦!
Akanipigia tena simu mara 5, mie kimyaaaβ¦!
Akaniandikia message nyingine:
"Best, nakupigia jamani pokea simu basi, nina pesa zako hapa nataka nikupeβ¦ Naomba basi tukutane mjini unisimulie vizuriβ¦!"
Mimi:
Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke kabisa mahala walipoβ¦!
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza na inasoma pesa zangu zote ninazo mdaiβ¦!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaβ¦. Kama sio mie vileπ