UDSM kilikuwa chuo kinachoheshimika sana. Wakati ule akina Walter Rodney wanafundisha hapo. Akina Neto, Frantz Fanon, Amilcar Cabrar na wana wengine wa Afrika wanakuja kutoa mihadhara hapo. Ilikuwa ukisikia profesa kweli ni profesa; na ukumbi wa Nkrumah ulikuwa ni ukumbi 'mtakatifu'