Hii ni dini ya kweli kweli na inayoenea kwa haraka. Mwanzilishi wake ni huyu dogo anayejiita Mfalme Adonis na anasema alitembelewa ndotoni na kuamriwa kuanzisha hiyo dini. Kujiunga ni bure ila kila mwaka inabidi ulipie ada ya dola 250 na ada ya maisha ni dola 3,000.
Sala zao zinajumuisha wanawake wenye misambwanda kutoka duniani kote na zinahusisha twerking na mengineyo...
Mfalme Adonis ametoa kitabu "kitakatifu" cha dini yake. Kitabu hiki kinauzika kwa haraka sana na kukipata Amazon ni kwa kubahatisha tu. Kuna mvuvumko mkubwa wa dunia nzima kupenda misambwanda na kanisa hili japo ni changa lakini limevutia watu wengi sana na linakua kwa kasi.