Vituko mitandaoni. Tupia chako

Umenikumbusha nilivyokuwa darasa la tatu tulipangwa wanne kwa dawati moja bahati mbaya dawati zote zikaenea nikabaki mimi pekee yangu, mwalimu akaniambia nitafute dawati lolote nikae.
Kila mtu alinikataa nikakaa chini, jumapili nikaenda shuleni nikaenda darasa la saba kule ni kuchukua dawati nikaenda kulitenga nyuma kabisa darasani kwetu.
Jumatatu kila mtu anashangaa nimetoa wapi dawati, wakati wao wanababana mimi nimejiachia mwenyewe kwenye dawati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…