Vituko mitandaoni. Tupia chako

Jamaa kaamka asubuhi, kavaa track suit na kumuamsha mkewe BETTY


JOHN: Amka twende jogging mke wangu?

BETTY: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa?


JOHN: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya.

BETTY: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa?


JOHN: Basi yaishe endelea kulala

BETTY: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?


JOHN: Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby

BETTY: Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?

JOHN: Jamani mi sijasema hilo

BETTY: Kwa hiyo mie muongo?

JOHN: Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii

BETTY: Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?


JOHN: Sikia we lala mie naenda jogging.

BETTY: Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"


JOHN: Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu
BETTY: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe...

JOHN: Basi ngoja tu nilale siendi jogging
BETTY: Kwahiyo ulikua unanijaribu?


Wanawake Mungu anawaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…