Unafiki tu. Ukiona nukuu zake zimeshiba sana wakati matendo yake mwenyewe yalikuwa kinyume. Katiba hiyo anayoilalamikia yeye mwenyewe, kwa kiasi kikubwa, ndiye mtunzi. Kama aliona kweli ilimpa madaraka makubwa sana mbona asingeibadilisha tu na kujipunguzia? Tena wakati ule alikuwa peke yake hakuna cha vyama vingi wala nini; na neno lake ndo lilikuwa la mwisho.