Vituko mitandaoni. Tupia chako


DAR: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mara kadhaa Rais Samia amekuwa akichafuliwa Mitandaoni lakini amekuwa kimya huku akisisitiza yasichukuliwe maamuzi yatakayowadhuru Raia

Nape amesema “Kuna jamaa fulani walimshambulia sana Rais na Familia yake kwenye Mitandao, huku ndani wakaanza kuuliza tunafanyaje? Mjadala ukawa mkubwa tuwachukulie hatua. Tukasema kwa hawa au kwa jukwaa lote lililotumika?”

Ameongeza “Lakini wakati majadiliano yakiendelea, Rais Samia aliniita na kuniambia nataka utatue jambo hili kwa busara. Nilitangaza 4R, mojawapo ni kuvumiliana, hata kama mnataka kufanya lolote, hakikisheni hamuingilii Uhuru wa Watu kujieleza."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…