Vituko kesi ya Lema vyaendelea............Part 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko kesi ya Lema vyaendelea............Part 2

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 17, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hadi kesi itakapoisha tutajionea kila aina vituko katika kesi hii

  Baada ya Juzi Lema kuanza kuhutubia mahakamani kwa kusema Pipoooozzzzzz......., Safari hii Jaji Gabriel Rwakibarila amegeuka kuwa kituko mahakamani ambapo jana Ijumaa wakati kesi ikiendelea alikuwa akiwaamsha wale wote waliokuwa wanaosinzia mahakamani na kuwapa adhabu palepale huku wasikilizaji wakivunjika mbavu.

  Kitendo hicho ambacho kilikuwa kikiwavunja mbavu watu wlaiojitokeza kusikiliza kesi, kilitokea mara kadhaa ambapo jaji Gabriel alikuwa akimuona mtu anasinzia, alikuwa akimwamsha na kumpa adhabu ya kusimama kwa dakika kadhaa palepale alipo, na baada ya muda huo kupita alikuwa anarukusiwa kukaa kuendelea kusikiliza kesi hiyo huku wasikilizaji wakivunjika mbavu.

  Tusubiri vituko zaidi katika kesi hii.

  Source. Gazeti la Mwananchi
   
 2. a

  abujarir Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahaha! ukistaajabu ya musa utaona ya firauni haya kwa mbali yanakaribiana na yale ya peoples power kwenye mazishi ya marehemu j.sumari
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hii kesi inaweza kuchukua rekodi ya kuwa kesi yenye vituko kuliko zote
   
 4. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa sababu madai ya kesi tu ni kituku..wakaanga vitumbua wanataka kupinga ushindi wa mbunge wao.
   
 5. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimependa maamuzi ya Jaji.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Peter Saramba, Arusha
  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, jana aliiomba mahakama kutupilia mbali tuhuma dhidi yake kwa sababu ni za uwongo, chuki na fitna.

  Amedai kuwa hali hiyo ndiyo iliyowafanya Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa na aliyekuwa mgombea kupitia CCM, Dk Batilda Burian, hawakufika mahakamani kutoa ushahidi licha ya kutajwa mara kadhaa.

  Akiongozwa na wakili wake, Method Kimomogoro katika kutoa ushahidi, Lema alidai kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa na wapiga kura watatu, imetokana na chuki za mlalamikaji wa kwanza, Mussa Mkanga baada ya kukosa udiwani katika Kata ya Sombetini.
  Alimwomba Jaji Gabriel Rwakibarila kuwaamuru wadai kumlipa ghrama zote alizoingia na muda wake aliopoteza tangu alipoanza kuhudhuria shauri hilo lililoanza kuunguruma Julai mwaka jana, ili iwe fundisho kwa watu wengine.

  Alimweleza jaji kuwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ya kibunge, kwa sababu ameazimika kuhudhuria mahakamani kushughulikia kesi hiyo.

  Alidai kuwa kesi hiyo imetokana na madai ya uwongo uliotungwa na wadai Mkanga na wenzake Agnes Mollel na Happy Kivuyo wanaowakilishwa na mawakili Alute Mughwai na Modest Akida.

  Aliieleza mahakama kuwa kama tuhuma dhidi yake zingekuwa za ukweli, Lowasa na Dk Burian waliotajwa kwa namna ya kuonekana kudhalilishwa na kushushiwa hadhi yao mbele ya jamii, wangefika mahakamani kutoa ushahidi ili kuthibitisha tuhuma dhidi yake.

  Lema alidai viongozi hao wameacha kwenda mahakamani kutokana na ukweli kwamba maneno yanayodaiwa kuwa aliyatamka dhidi yao si ya kweli.

  Alidai kuwa hiyo pia ndiyo sababu ya Dk Burian kutofungua kesi dhidi yake baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

  Aliieleza mahakama iliyojaa wasikilizaji kuwa hata katika barua yake ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi, Dk Buriana alishindwa kuorodhesha au kutoa mifano ya kauli za matusi, kashfa na udhalilishaji alizodaiwa kuzitoa.
  Lema alidai kuwa kitendo hicho ndicho kilichomlazimisha msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Arusha Mjini, Raphael Mbunda kumruhusu kuendelea na kampeni.

  Shahidi hiyo alidai hata vielelezo vya nakala ya CD zizodaiwa kurekodiwa maneno yake ya matusi hayakuwasilishwa mahakamani kuthibitisha tuhuma dhidi yake.

  Alidai kuwa CD hizo zingewasilishwa mahakamani kesi hiyo ingekuwa imeisha mapema kwa sababu ukweli ungedhihirika.

  Katika hatua nyingine, Jaji Rwakibarila aliendelea kuwavunja mbavu kwa vicheko wananchi wanaohudhuria mahakamani baada ya jana kuanza mtindo mpya ya kudhibiti wanaosinzia wakati kesi inaendelea kwa kuwaamuru kusimama kwa dakika kadhaa kabla ya kuwaruhusu kuketi tena


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwanza wale waliofungua tu ile kesi ni VITUKO SANA.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye red ni mateja product ya mh.LEMA.
   
 9. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu lakini si wapiga kura pia na walimsaidia kushinda au?...Halafu kama CCM walishindwa kuwarubuni mateja wauze shahada zao za kupigia kura na kupelekea Batilda kushindwa vibaya basi CCM wana kazi kubwa sana mbele ya safari.
   
 10. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  peoples power imemkaa rema akilini ndo maana hata kwenye mazishi ya sumari alisema aliposalimia.
   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hivi ni kosa kulala mahakamani??
   
 12. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...ukiona hivyo ujue jaji Gabriel kaishaona hapo hakuna kesi kwa-hiyo ili watu wasiboeke kaamua kuwachangasha,muda uishe atoe ukumu ya kuitupilie mpali hilo likesi la kubumba...
   
 13. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  basi tujiandae na hukumu ya washtaki kulipa fidia
   
 14. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,573
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ns mimi pia... Kweli unambwato mnduku we.......gamba nchemba....
   
 15. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  ukiona wakili anasimamia kesi alafu wanaenda mahakamani anakimbiwa na mashahidi ujue kazi ipo
  itakuwa fundishao kwa wale waliozoea kumega haki za watu kama wanamegwa kitandani
  Pplzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz P...................
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ELIMU YA LEMA!.
  Imebainika kuwa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ni 'KIHIYO', hayo yamejiri mahakamani ktk kesi inayoendelea ya kupinga matokeo ya ubunge wa Lema. Akihojiwa na wakili wa wadai Alute Mughway Lema alishindwa kuielezea mahakama kiwango chake halisi cha elimu kinyume na alivyojaza ktk fomu ya tume ya taifa ya uchaguzi na katika kumbukumbu za ofisi ya bunge ambapo fomu hizo zina├Ânyesha Lema alimaliza darasa la 7 mwaka 1989 na kujiunga sekondari 1989-1992 (miaka 3) na kuonesha kujiunga na 'A- level' mwaka huo huo wa 1992-1993 (hakunaga) na pindi alipobanwa na wakili Mughway alikiri kuwa hakumaliza kidato cha nne bali aliishia kidato cha tatu tu. ambapo alitakiwa aeleze aliwezaje kwa hali hiyo kusoma A-level AKAJICHANGANYA, Pia lema alipata wakati mgumu na kushindwa kutoa maelezo ya madai yake ya kuwa na diploma ya CAMBRIDGE COLLEGE ambapo alishindwa kuielezea mahakama nini maana ya diploma, pia kutokujua chuo hicho maarufu kilipo. Huyu ndio Godbless Jonathan Lema 'MPIGA DILI' wa Arusha ambaye pia eti ni 'WAZIRI KIVULI MAMBO YA NDANI'...Ama kweli "ELIMU YA MJINGA NI MAJUNGU... IKIWA UNAONA ELIMU NI GHALI BASI JARIBU UJINGA"!.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  nikiwa Arusha kipindi hicho cha miaka hiyo, 98% ya wanaosoma kolila walikuwa wanakula "gwee" "ndumu" au bangi au Msuba, shule nzima kama kuna divsion 3 basi huyo kipanga. wengi "0" wanazungusha ile ya point 35
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  ‎"Awali hoja kuhusu utata juu ya elimu ya mbunge huyo iliibuka baada ya wakili Mughwai kuhoji taarifa zake za elimu zilizopo katika kumbukumbu za nyaraka za bunge, hoja iliyojibiwa na shahidi huyo kuwa imetokana na makosa ya uchapaji uliosababishwa na Bunge lenyewe akidai tayari aliiandikia ofisi ya Bunge kuelezea hilo na kutaka marekebisho".15 March 2012

  Peter Saramba, Arusha | Mwananchi
   
Loading...