Vitu vya kuzingatia kabla ujaanza biashara

demarine

Member
Dec 6, 2020
18
29
Upatikanaji wa kazi kwa sasa umekua ni mgumu kila sehemu watu wanaangaika kutafuta ajira ili wapate kipato na kujiinua kiuchumi ili maisha yaende ,wasomi kwa sasa wamekua wengi kira kona kuna vyuo jambo ambalo linapelekea kuwa na wasomi wengi wasio na ajira.Kutokana na ili tatizo watu wengi wameamua kujikita katika biashara ndogo na kubwa ili kukabiriana na ili tatizo, Lakini kumbuka kabra ya kuanza biashara yoyote kuna mambo yakupasa kuzingatia ili usipoteze pesa yako au ukaingia kwenye biashara ambayo itashindwa kukupa unachoitaji.

1. WAZO
kabra ya kufanya biashara kitu cha umuimu au ni lazima uwe nacho ni wazo la biashara , wazo linaweza likawa ni jipya au umelitoa kwa watu wengine ,mara nyingi mawazo ya biashara uwa sio mapya ila kikubwa akikisha kama ni wazo la mtu ufanye uchunguz je linamlipa na mazingira anayo fanyia yanafanana na unapotaka kwenda kuanzisha biashara nikiwa na maana ya upatikanaji wa wateja pia yakupasa kuwa mbunifu, ongeza vitu vya ziada ambavyo wengine awatoi mfano punguzo la bei na ubora wa bidhaa au huduma ili kufanya wateja wanunue bidhaa zako.Na mwisho akikisha je wazo lako linakubarika kisheria au la ili usiingie migogoro na serikari.

2. FANYA UNACHOKIPENDA
hili ni jambo la umuhimu sana watu wengi wanafanya biashara kwasababu wanaona wenzao Wanapata faida bila ya kujua changamoto wanazopitia, kwaiyo akikisha unafanya kitu unachokipenda hii itakusaidia kuwa mvumilivu maana kuna mda biashara inaweza isiuzike kama ulivyo fikiria kwaiyo yakupasa kuwa na uvumilivu mpaka wateja watakapo kuzoea. Unapochukua chaguo lisilo sahihi tegemea kufeli tu.fanya unachopenda usifate watu wanafanya nini.

3. MWONEKANO WAKO NA MAZINGIRA
Mwonekano wako jinsi unavyo jiweka pia ni muimu ktk ufanyaji wa biashara ukiwa smart itasaidia kujenga imani juu ya wateja wako, unapojiweka lafu wateja watakosa imani ya ata unachokiuza wataamini sio kisafi. Pili mwonekano wa mazingira ya biashara, ili ni jambo la umuimu sana wateja wanavutiwa na mazingira ya biashara unapokuwa na mazingira safi na yakuvutia wateja watakuja sana kuitaji uduma zako.Kwaiyo akikisha unajiweka ktk hali ya usafi wako na mazingira ya kazi kama ni kibanda jenga chenye mvuto.

4. ELIMU YA BIASHARA
Akikisha kabra ya kuanza biashara uwe na elimu ya kutosha juu ya biashara unayotaka kuifanya kuriko kukulupuka alafu badae ukaanza kusema ningejua, fanya utafiti kuhusu unachotaka kufanya jifunze kwa ambao wanaofanya pita kwa watu kazaa uliza,jifunze jinsi ya kufanya ,changamoto za iyo biashara na faida zake ,jinsi ya kupata material na kadharika, hili litasaidia kupunguza kauri ya ningarijua.

5. WATEJA
Biashara bila wateja sio biashara ,kabra ujaanza biashara akikisha unafahamu aina za wateja ambao wanaitaji iyo bidhaa ,tuna makundi 3 ya wateja ambayo ni watoto,vijana na wazee kwaiyo yakupasa kujua bidhaa yako ina lenga group lipi na unawezaje kuwa handle, heshima pia ni kitu muimu akikisha una kauri nzuri kwa wateja ili kesho walud tena kwako.

MWISHO
Kwa haya machache natumaini umejifunza kitu, pia kama una chakuongezea please add your comment lengo tujifunze wote, karibuni.......
images.jpg
 
Muonekano sio ishu kwenye biashara, labda biashara za matozi tu;-
fika kabwe ple kwenye maduka ya hardware unakuta mabosi kina mgwaasi, machemba n.k wanashindia maovaloli tu lkn jioni kufunga hesabu ya 100mili uwakika...
 
muonekano sio ishu kwenye biashara, labda biashara za matozi tu;-
fika kabwe ple kwenye maduka ya hardware unakuta mabosi kina mgwaasi, machemba n.k wanashindia maovaloli tu lkn jioni kufunga hesabu ya 100mili uwakika...
Kuhusu muonekano Hua inategemeana na aina Ya biashara mkuu, mfano ukifungua mgahawa lažima mazingira yawe masafi na muonekano Pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom