Vitu 3 Ambavyo Vitafanya Tangazo lako la Biashara Lifanikiwe au Lifeli Online

Aug 22, 2022
9
8
Nimefanya kazi ya Kutengeneza Matangazo ya Wafanyabiashara pamoja na Matangazo yangu binafsi...

Naweza kukuambia kama Unahitaji Tangazo lako Lifanikiwe au Lifeli

Basi zingatia/usizingatie Vitu hivi 3 unapofanya Matangazo yako


1. Muonekano wa Tangazo

Hapa nimetumia muonekano kwa sababu Mtandaoni watu wanaanza KUONA ndio WANASOMA (Au hawasomi)

Hivyo kama unataka kukamata Attention ya watu wanaopita Mtandaoni na wawe Interested na Kitu chako...

Hakikisha Kinaonekana vizuri kwanza,

Na hapa namaanisha iwe ni Picha, Video au Poster zimedizainiwa... Hakikisha zinavutia kuangalia kwa macho.

Wafanyabiashara wengi wanapatia hapa.. Ila kama unaona kwako wewe bado,

Jitahidi Ku improve Quality ya Matangazo yako kwanza (Muonekano wake)


2. Maelezo ya Tangazo (Ad copy)

Hapa sasa ndio kimbembe...

Na sio kwamba Wafanyabiashara wengi maelezo wanayoandika hayaeleweki..

No,

Maelezo Yanaeleweka.. Lakini hayana nguvu ya USHAWISHI

Ukweli ni kwamba Biashara ya Kuuza Mtandaoni inahitaji mbinu za ushawishi..

La sivyo, utakuwa huuzi kabisa....

Au unauzia watu wachache tu na kuishia kulalamika hupati Wateja kila siku

Kumbe maelezo yako hayana Ushawishi.. Watu hawavutiwi hata kuyasoma

Unakuta Unaandika Bidhaa..Bei.. location umemaliza...

Wengine hata bei hawaweki utaskia "DM for price"

Kuna kitu Kinaitwa COPYWRITING...Je unakifahamu?

Kama mfanyabiashara wa Dunia ya Leo, ujuzi wa kuuza katika Maandishi ni wa muhimu sana

(Don't worry kama haufahamu kabisa... endelea kufuatilia posts zetu,Utajifunza soon)


3. Walengwa wa Tangazo (Target Audience)

Ukizingatia namba 1 na 2 hapo juu, halafu ukafeli hapa.. Pole sana

Just imagine,

Uko na Tangazo zuri na lenye maelezo mazuri... Lakini linaonekana kwa watu ambao sio sahihi..

Je, Utauza kweli?

Hapana,

Siri ya kwanza ya kuuza Mtandaoni ni kuonesha Biashara yako kwa watu sahihi

Yaani Watu ambao wana uhitaji na wanaweza kununua...

Sio kukupotezea muda wako.

Jifunze Kutengeneza Target Audience ya kuonesha Matangazo yako.. Hata kama unaboost post tu

Utaona Matokeo yake,

Note: Ukitumia Ads Manager ndio inakuwa Unyama zaidi

Vitu hivi 3 vinachangia Sana katika kufanikisha Tangazo lolote lile la Mtandaoni

Unaweza Kuzingatia/Puuzia ... At your own risk
.

.

.
Je,unapenda kujifunza zaidi kuhusu Social Media Marketing,Sponsored Ads na Biashara Mtandaoni kwa ujumla?

Basi Jiunge na Group letu la Mafunzo ya BURE kwa Wafanyabiashara

Tuma Ujumbe "ADD ME" kwenda Namba hii ya WhatsApp 0627401779

Ambatanisha Na Jina lako + Biashara unayofanya

Nitakuadd

.
.
.
Tukutane ktk Somo lijalo. ..

Kama una swali lolote hapa, usisite kuuliza
m19.jpg
RATIBA-MATANGAZO-ACADEMY.jpg
Screenshot_20220903-105457.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom