Vitisho vingi vinaibeba UKAWA

Vitisho vingi vinaibeba UKAWA

chikub

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
110
Reaction score
28
Wana CCM ni wapenda amani hata kama ni masikini. Hawapendi vurugu kwakuwa wengi wao wanatoka kwenye kundi la watanzania wenye vitu vingi vya kupoteza kama ikitokea vurugu mitaani na nchini. Wengi wao ni watu wenye mali kama vile familia, watoto, wajukuu, nyumba, mashamba, magari, ajira na ndugu na jamaa wenye nafasi nzuri kikazi.

Mara nyingi kundi hili huwa linaepuka na kukaa mbali na sehemu yenye vurugu ili kulinda walichonacho kisiharibiwe, na wangine wanaweza hata kuikimbia nchi kwa muda.

Kundi hili ni rahisi sana kutishwa na maneno, matamko na vitendo vya watawala, taasisi, polisi, askari, tume, viongozi wa dini na vyama vya siasa vinavyoashiria uwezekano wa kutokea vurugu mahali fulani. Wanaweza wasijitokeze kwenda kupiga kura wakiona polisi na askari wengi mitaani.

Tofauti na wafuasi wa UKAWA na vyama vingine vya upinzani ambao wengi wao wanatoka kwenye kundi la watu wasiokuwa na vitu vingi vya kupoteza hata kama ikitokea vurugu mitaani. Wengi wao hawana familia, ajira, nyumba, magari, wala ndugu na jamaa wenye nafasi nzuri serikalini.

Kundi hili ni la vijana na watu wazima ambao maisha yao ni yakubangaiza, hivyo vurugu ikitokea kwao ni sehemu ya mafanikio kwao. Na mara nyingi huwa wanaelekea kulekule zinakotokea vurugu hizo, huenda wakaokota kitu.

Hili sio kundi la watu wanaotishika kwa urahisi kwa matamko na kauli za mtu au chombo chochote. Hili ni kundi ambalo lina uwezo wa kwenda kupiga kura hata kama polisi wenye bunduki wako wengi vituoni.

Serikali, tume, viongozi wa dini na vyama, polisi, wanajeshi na wadau wengine acheni kutoa vitisho vingi kwa wananchi ili kutoa fursa kwa wanawake, wazee, matajiri, wenye familia, na walemavu wapate hamu ya kujitokeza kwenda kupiga kura. Kauli kali, polisi na askari wengi mitaani ni mtaji mkubwa kwa vyama vinavyoungwa mkono na vijana na watu wazima maskini.

Waelimisheni watu msiwatishe, fuateni sheria badala utashi wa mtu au kikundi, na hubirini haki, uhuru na amani kwa wananchi ili kuepusha vurugu kutokea. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hakuna duniani vitisho, polisi wala jeshi lililofanikiwa kupambana na umma wa watu wake likashinda vita hiyo. Ni haki tu iliyofanikiwa kuleta mafanikio sio jeshi.

Yangu macho tu.
 
Lowassa Kwisha habari yake.

Umesoma Alicho Andika Mleta Mada? Au Ndiyo Kukurupuka? Kuliko Jaa Ushabiki Wa Kijinga Tena Kushabikia Ujinga Unaofanywa Na ccm Kwa Kutaka Kuwaaminisha Wananchi Kwamba Wao Siyo Wastaarabu Ni Watu Wavurugu?

Unajua Athari Ya Ujinga Huu Unaofanywa Na Chama Cha Mapinduzi Kuchochea Chuki Baina Yao Na Wananchi?

Unajua Uzalendo Unajengwa Kwa Haki Na Usawa? Kama Haya Hakuna Amani Kuwepo Ni Ndoto, Amani Itakayo Kuwepo Ni Amani Ya Kulazimishwa na Siyo Amani Inayotoka Mioyoni Mwawatanzania Aliyoitengeneza Baba wataifa, Kwa Hiyo Unaposhabikia Uwe na Ufahamu Wa Unachoshabikia.
 
Nakubaliana na wewe.......

Kwa waliodhamiria kupigia kura UKAWA wengi hawawezi kuacha kwenda kupiga kura kwa hizi kauli za vitisho.......labda hili la mita 200 kuna baadhi wataenda kuendelea na mambo yao mengine na vile vile kuna ambao watabaki hizo mita 200 no matter what.

Wana UKAWA wengi tumekuwa tunaisubiri siku ya tarehe 25 October 2015 kwa hamu sana na hakuna namna eti tukaacha kwenda kupiga kura sababu ya kauli za vitisho.....

Ambao wanaweza kuogopa mostly watakuwa ni wapenzi wa CCM, kwa hiyo kauli hizi za vitisho in terms ya kupunguza wapiga kura itaa-affect upande wa CCM negatively.....
 
Back
Top Bottom