Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Ni vibaya ya kwamba kwa sababu ya kukosa fedha watu wengi katika nchi za joto wanateseka
kwa kutokana na njaa. Lakini pia ni vibaya zaidi ya kwamba wanateseka ya kuwa jibu la
kupata matangazo yanayoshawishi kununua vitu vilivyotengenezwa kama kiamsha hamu
(appetizer)juisi ya vitamini nk. Vitu hivi havina faida na sio lazima. Nyama ni rahisi na
inakupa nguvu zaidi kuliko kichupa cha sana-vita-liver extract. Vitamini za kurutubisha za
Emajani yake yana nguvu zaidi kuliko Paradiaso impotexvidonge vyake.
Mama mmoja kutoka kijiji chetu D.R. Kongo alitumia mshahara wake kwa wiki nzima, kwa
ajili ya chupa moja ya sirapu nyekundu iliyotengenezwa bandia, akiamini itamsaidia binti
yake kumwimarisha damu. Mwanamke huyu alikuwa kirahisi mwanakijiji? Hebu tuangalie
kwa karibu katika jiji na Hospitiali za kanisa, hata katika miji mikubwa.Kuna ufujaji katika
bajeti, katika bajeti vitu kama hivyo kama sindano za vitaminivitamini B za vidonge,
vitamini E tortehaemo-vit-orangena vingine vitolewavyo na kupendwa kwa majina.
Watu wahusika wangefanya vizuri zaidi kuweka machungwa na karanga katika mashelfu yao
maduka ya madawa!
a)Vitamini A: Muhimu kwa ajili ya macho na kwa ajili ya utando na ngozi (skin).
Inapatikana katika rangi zote nyekundu na rangi ya manjano, matunda na mboga; Mapapai,
Karoti, Nyanya na Maembe; katika mayai na katika matunda ya mchikichi. Mafuta ya
mchikichi ni tajiri sana katika vitamini A. Huko Afrika ya magharibi, mahali ambako kuna
wingi wa mafuta ya mchikichi, watu wachache wanateseka na upofu. Katika mashariki na
kusini mwa Afrika ambako mafuta ya mchikichi ni haba, tunapendelea kukuza na kula
machungwa, viazi vitamu, kuepuka mahitaji ya vidonge vya vitamini A.
b)Vitamini B komplex: Muhimu kwa ajili ya wale wenye matatizo ya usumbufu wa mishipa
na kudhoofika. Vitamini hizi ni za lazima kwa ajili ya kuyeyusha na kufyonza kabonhaidreti
kama sukari, unga. Vitu vilivyotengenezwa kienyeji vipatikanavyo, kama Karanga,
Maharage
ya soya, Maharage, Nyama, Samaki, Hamira, mboga za majani na mchele makapi au maziwa
ya mama yaliyo na kiasi kikubwa cha vitamini hizi. Ni kosa kubwa , kwa sababu hii kuuza
Karanga ili kununua vitamini Bbiskuti.
c) Vitamini C: Kinga asili ya mfumo wa miili yetu, ambayo inatukingia maambukizo
alimradi vitamini C. Watoto wa umri hadi miezi 6 wanapata ya kutosha maziwa ya mama zao.
Zaidi ya umri huu mmoja ni lazima ale aina zote za matunda (hasa machungwa, matunda ya
karakana na malimao) na mboga za majani (mboga za majani, vitunguu na viazi n.k). Mtunda
yasiyopikwa na mboga ni bora zaidi kwani yakipikwa yanapoteza vitamini C. Tofauti yake na
vitamini A, vitamini C haiwezekani kuhifadhika mwilini, kwa sababu hiyo ni lazima kula
matunda na mboga kila siku.
d) Vitamini D: Inasaidia katika kukua kwa mifupa. Mwili wenyewe unatengeneza kutoka
jua. Mayai na mafuta pia ni chanzo kizuri toka vitamini D.
e) Vitamini E: Inapatikana kutoka majani mabichi na mafuta ya chakula. Utendaji kazi
kiafya bado haueleweki kamili. Katika utangazaji inaitwa vitamini ya uzazi wa watoto
lakini hata hivyo, hakuna mgumba aliyepata watoto na kushukuru vitamin E kimadawa!