Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,857
Kumekuwepo na taarifa za kukamatwa kwa matani ya sukari kwenye maghala ya wafanyabiashara sehemu mbalimbali nchi lakini tatizo la sukari mdio linazidi kuwa kubwa.
Kwa mfano,hapa Dodoma napoishi jirani kabisa na town centre(mwendo wa robo saa tu kwa mguu kufika town) maduka hayana sukari na wenye maduka wanakwambia wao hawawezi kununu sukari mfuko wa kilo 25 kwa shilingi 80,000 alafu waje wauze kwa bei elekezi ya shilingi 1800 kama walivyoagizwa na watendaji,na viongozi wengine wa serikali za mitaa.
Nimejaribu kumhoji muuza duka mmoja akaniambia ili waweze kuuza sukari kwa bei elekezi,basi wanapaswa kuuziwa mfuko wa kilo 25 kwa shilingi 35,000 na sio shilingi 80,000.
Sasa najiuliza hawa wanaouza hiyo sukari kwa shilingi 80,000 kwa mfuko wanauzia sukari hiyo mwezini kiasi kwamba ni vigumu kuwabaini?
Hizo tani za sukari zilizokamatwa zimeenda wapi?
Na je,sukari iliyoagizwa na serikali nayo imesaidia nini mpaka sasa kushusha bei hii?
Je,wenzangu hapa JF, huko mtaani kwenu upatikanaji wa sukari ukoje?