illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Nchi za Marekani ya kusini ndio zinatikisa sana kwa matumizi na biashara hii, wahusika wa madawa haya huwa wana makundi yao kama majeshi ya kuwalinda (violent drug gang)ambapo ukisikia muuza madawa anaenda kukamatwa ujue ni mirindimo ya silaha nzito kwa muda hata wa wiki vita hii huwa ni kati ya vikosi vya usalama vya serikali na vikosi vya hawa drug gangs kuna jamaa alikuwa anaitwa Christopher dudus huyu ni mjamaica sasa kafungwa huko Marekani ila siku ya kukamatwa kulikuwa na maandamano makubwa sana nchini Jamaica hii ni kwa sababu hela zile za madawa alitumia kufanya shughuli nyingi za kijamii kama kujenga mahosipitali mashule na huduma zingine ambazo serikali haina ni sawa na hapa nchini kwetu kujenga hosipitali ya figo....nazungumzia mtu mwenye chumba kilicho jaa dola (kumbuka hela za madawa hazikai benki)mtu mwenye kikosi cha wanamgambo wenye mafunzo na silaha za maana unaweza kufananisha vita hii na hawa kina nanihi wetu wa bongo hapa ambao unatangaza kwenye vyombo vya habari kabla hujamaliza unakuta wameshajipeleka central police
Angalia hii video hapo ni siku ya tano wanahangaika kumkamata mtu
Angalia hii video hapo ni siku ya tano wanahangaika kumkamata mtu