maonomakuu
JF-Expert Member
- Jul 24, 2015
- 2,516
- 1,198
Vita kati ya serikali ya Magufuli na watumishi wa umma ni vita vikali sana ambayo binafsi nayaunga mkono kama yanazingatia sheria za Utumishi wa umma.Serikali inawaaminisha wananchi kwa nguvu zote kuwa tuko hapa kwa sababu ya watumishi wa umma wasio kuwa waaminifu, sina shaka na hili ni kweli kabisa lakini tutafakari mambo haya.
Nani anawateua hao watumishi ambao wanawasimamia watumishi walio chini yao? bila shaka ni mamlaka za juu za serikali sasa hao wateuzi kwa nini wasijiwajibishe wenyewe maana wameshindwa kuwasimamia waliowateua?Serikali hawapeleki bajeti zilizokadiriwa za maendeleo na matumizi mengineyo sasa mipango iliyopangwa na serikali itafanikiwa vipi piñdi zinapelekwa 20% ya bajeti kwa mwaka?
Watumishi wa umma wanaingiliwa sana kimaamuzi na wanasiasa sasa utegemee kazi zitaenda kama zilivyopangwa?Madai ya watumishi wa umma kwa serikali siyo tatizo na malipo ya upendeleo baini ya serikali za mitaa na kuu huku mashirika ya umma yakineemeka kupata mishahara mikubwa alafu utegemee utendaji unaofanana?
TUCTA wanawatetea watumishi wa umma lakini serikali imeweka pamba alafu mnataka Utumishi uliotukuka.
Rais wangu Magufuli kaa na TUCTA vema uwasikilize alafu tatua changamoto za watumishi wa umma alafu wasimamizi wao kao nao kwa umakini ili watumishi warudi kama enzi za Nyerere kujiona ufahari katika Utumishi wa umma.
Tuache kauli za vitisho maana hazijengi.