Vita Kali: Samwel Sitta Vs Maaskofu

Vita Kali: Samwel Sitta Vs Maaskofu

Baada ya samwel sitta kula chakula chake na kuropoka...sijui alikula maharage ya wapi huyu...mh Edward ngoyai Lowassa alimuombea msamaha sitta viongozi wa dini waliotukanwa wakakutana kujadili kauli hiyo ya Lowassa
 
Nilishawahi kusema, kwa sasa hakuna mwanasiasa mnafiki na mwenye chuki kama Sita..... Sita akiona madaraka mbele yake anaweza hata kumsaliti mke wake

Nasikia kuna wakati alitaka kubadilisha jinsia ili apewe uspika.

Huyu mtu ni hatari sana, lakini kuna hatari iliyojificha nyuma yake nayo ni "Ndege wanaofanana huruka kundi moja"

Huyu sita ana "manyoya" sawasawa na wana ccm wote nchini, nadhani mnauona ukubwa wa hatari!!!!!
 
sita na pengo wamejiondolea heshuma waliyojijengea miaka mingi kwa kukosa busara tu kuhusu katiba hii pendekezwa.
 
* KWA NINI WATANZANIA TUMCHAGUE MGOMBEA URAIS ANAYETUKANA VIONGOZI WA DINI?

Kweli duniani kuna maajabu mengi. Na katika nyakati hizi maajabu yanazidi kuongezeka kila kukicha... Nani alitegemea yule mwanasiasa aliyediriki kuwatukana wachungaji leo hii awe na ujasiri, dhamira na ndoto ya kugombea urais..

Pamoja na kutaka kwake urais ni jambo la wazi Samwel Sitta amejiweka katika wakati mgumu pale alipozua mgogoro mpya dhidi ya viongozi wa dini ya kikristo. Hii ni baada ya kuita waraka walioutoa wakristo kuwa ni wa kijinga, kipuuzi na wa ovyo..

Kama tunavyojua ujumbe/waraka wa viongozi wa dini ni wa kinabii wenye maslahi mapana kwa wananchi ila ni Samwel Sita huyu huyu aliyeita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi, kijinga na ovyo... Tafsiri yake ni kwamba viongozi wa dini saizi wamekuwa wa ovyo, wapuuzi na wajinga mpaka watoe waraka wa kipuuzi na ovyo, watanzania tusimame pamoja kukemea tafsiri hii ya Sita kwa viongozi wetu wa dini...

Kitendo hicho kiliwafadhaisha na kuwakasirisha maaskofu kitendo kilichopeleka maaskofu hoa kumfananisha Sita na Goliati wa kwenye Biblia aliyeshindwa na Daudi kwa sababu ya jeuri, kiburi na matusi kwa Mungu.

Naomba ikumbukwe kipindi cha bunge la katiba Sita alitoa maneno ya dharau, kejeli, matusi dhidi ya viongozi wa dini wa kikristo, hasa jukwaa la kikristo, kauli hiyo ya Sita mpaka sasa bado ni mwiba mkali kwake, kwani iliwauzi na umeendelea kuwauzi viongozi hao....

Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karangwe, Dk. Ben Bagonza alipata kunukuliwa akisema "Nimemsikia Sita akitushambulia wachungaji... Sasa natumia hekima kumjibu kwamba maandiko matakatifu katika Biblia; 1 Samwel 17:36~37 hasa mstari wa 36 unasema, Goliati alipogombana Daudi ushindi wake ulitokana na Goliati kumtukana Mungu...

Na ukiona Goliati anaanza kumtukana Mungu, ujue ushindi wa Daudi umekaribia. Hivyo ndivyo Sita sasa anatukebehi na kututukana viongozi wa dini. Hapo tunakumbushwa na maneno ya Mungu yanayosema "Awatukanaye nyinyi niliowatuma amenikataa mimi" Tazama Luka 10:16", Alisema Askofu Bongaza (Tanzania Daima)...

Askofu jimbo la Katoliki la Bunda Mhashama Renatus Nkwande alisema "Kwa kweli Mzee Sita ametutukana, ametafuta ubaya kwa viongozi wa dini kwa kuwa tumesema ukweli! Sisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu wa wakristo..... Tulizungumza kutokana na hitaji la wakati na ulikuwa waraka wa unabii" alisema

Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini, Dk. Steven alisikika akijibu mapigo ya Sita kwa kusema "Hatuwezi kujibizana na mtu kama Sita bali tutaanzia pale atakapoishia. Ukibishana na mjinga utakuwa mjinga pia. Tunasubiri amalize kazi ya kula fedha za wananchi sisi viongozi wa dini tuna watu wengi zaidi (Tanzania Daima)....

Huyu ndiyo Samwel Sita, ambaye leo hii ana mategemeo, ana ndoto na dhamira ya kuwa kiongozi mkuu wa Nchi hii ifikapo Oktoba...

Mzee wangu Sita, kama unadiriki kutukana viongozi wa dini, je leo hii utapata wapi ujasiri wa kuomba kura zao na waumini wao?

Mzee wangu Sita, kama unadiriki kutukana viongozi wa dini ni kundi lipi litasaidia kuliombea Taifa letu?

Mzee wangu Sita, leo hii jamii unataka ikuelewaje hasa kundi la wakristo wakati ulishatukana viongozi wao wa kiroho?
Sitta kakosea sana , lakini hata kuwapa Rushwa Viongozi wa Dini ni dhambi kubwa
 
Ni Msukuma wa tabagaka la Kinyantuzu kutoka Bariadi waliyohamia Urambo kwa hofu ya ukoo wao kuwa wa kishirikina.

Eti ni kweli ni mjukuu wa Ng'wanamalundi? Yule legend wa kisukuma aliyekuwa anafanya miujiza?
 
Mzee 6 lugha yako dhidi ya viongozi wetu Wa dini itakuhukumu sisi waumini pia ulitukana waombe wapagani
 
Habari za sita ziliishia kwenye bunge la katiba.alijimaliza pale.hana issue katengeneza kura mpaka leo katiba yake imekosa utetezi inapingwa kila kona.
 
Kauli ya Kinabii, hizi dini ni mtihani kwa kweli. Mnataka kutuaminisha hata Maneno ya Gwajima kumtukana Pengo ni maneno ya Kinabii?
 
Sitta anaongea facts afu wewe unaleta opinion zako hapa ambazo ziko very biased! Acha kutumika na mafisadi wewe! Ukitaka nchi inyooke pigania yafuatayo...

Magufuli: Rais wa JMT
Sita: Waziri Mkuu
6 huyu wa kura za maruhani zilizo pitisha katiba ya kijani?
 
Mchakato wa katiba ni mwiba kwenye harakati zake kisiasa otherwise he he would make a good president
 
Back
Top Bottom